Meneja Mauzo Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) wa Mkoa wa Morogoro, Jemes Gomile(kushoto) akimkabidhi Vifaa vya michezo,Rais wa Chuo Kikuu cha ARDHI, Moyo Hamza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa hivyo kwa Vyo shiriki vya mashindano ya mchezo wa Pool kwa Vyuo vya Elimu ya juu Mkoani Morogoro.Katikati ni Mwenyekiti wa Chama cha Pool Mkoa wa Morogoro, Patrick Lugang’ha
KAIMU Kamanda wa
polisi mkoa wa Morogoro, John Laswai leo
atakuwa mgeni rasmi katika mashindano ya mchezo wa pool kwa wanafunzi wa vyuo
vikuu vya mkoani hapa ambayo yanajulikana kama 'Safari Lager Higher Learning Pool
Competition 2013'.
Akizungumza na
waandishi wa habari jana wakati wa
kukabidhi sare za kuchezea pamoja na fedha kwa ajili nauli na maadalizi kwa
vyuo vitakavyoshiriki, mwenyekiti wa chama cha mchezo huo mkoani hapa (MOPA),
Patrick Lugeng'ha alisema kuwa mashindano hayo yatakayoshirikisha vyuo vikuu
vinne yatafanyikia kwenye ukumbi wa Vijana.
Lugeng'ha alisema
kuwa mashindano hayo yanayodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia
bia yake ya Safari Lager yatafunguliwa na Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani hapa
na yatafungwa na Naibu Meya wa Manispaa ya Morogoro,Lydia Mbiaji.
Aliongeza kwa
kuvitaja vyuo vitakavyoshiriki mashindano hayo kuwa ni chuo cha SUA, Mzumbe,
Ardhi na chuo cha uandishaji wa habari (
MSJ).
Lugeng'ha alisema
kuwa mashindano hayo yatachezwa kwa mtindo wa chuo kwa chuo na mchezaji mmoja
mmoja wanaume na wanawake.
Alisema bingwa kwa
upande wa chuo licha ya kujinyakulia fedha taslim Sh.500,000 pia itakuwa
imekata tiketi ya kuuwakilisha mkoa huo katika fainali za taifa zitakazofanyika
kuanzia Juni mosi mwaka huu jijini Dar es Salaam, mshindi wa pili atazawadiwa
Sh.300,000, mshindi wa tatu Sh.200,000 na mshindi wa nne Sh.100,000.
Aidha alisema kuwa
bingwa kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja (wanaume) atajinyakulia Sh.150,000 na
tiketi ya kushiriki fainali za taifa, mshindi wa pili Sh.100,000, ambapo bingwa
kwa upande wa wanawake atazawadiwa Sh.100,000 na tiketi ya kushiriki fainali za
taifa huku mshindi wa pili akiondoka na Sh.50,000.





0 maoni:
Post a Comment