Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Rais
Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi tuzo maalum iliyotolewa na Taasisi ya
Chakula na Lishe kutambua mchango wake mkubwa katika kusimamia lishe na
maendeleo yake nchini katika uzinduzi wa kampeni ya lishe nchini leo Machi 16, 2013 katika bustani ya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam. Kulia ni Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na kushoto ni Mama Salma Kikwete akifuatiwa na Mama Maria Nyerere
Mama Maria Nyerere akifurahia
tuzo maalumu aliyopokea kwa niaba ya Baba wa Taifa aliyotunukiwa na
Taasisi ya Chakula na Lishe kwa mchango wake mkubwa kwa kukuza na
kuendeleza sera ya lishe nchini wakati wa sherehe za uzinduzi wa Kampeni
ya Lishe Tanzania leo Machi 16, 2013 katika bustani ya Mnazi Mmoja
jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Naibu Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid akisalimiana
kitabu cha kampeni ya Lishe Tanzania baada ya kukizindua leo Machi 16,
2013 katika bustani ya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam. Kulia ni Rais
Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na kushoto ni Mama Salma Kikwete
akifuatiwa na Mama Maria Nyerere
0 maoni:
Post a Comment