Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando Akiongea na
waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa TFF wakati wa kukabidhi
vifaa vya michezo kwa ajili ya timu zinazoshiriki mashindao ya vijana
chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars mwaka huu
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando (kushoto)
akikabidhi vifa vya michezo kwa Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF Sunday
Kayuni na Mwenyekiti wa DRFA Almasi Kasongo kwa ajili ya timu
zinazoshiriki mashindao ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel
Rising Stars mwaka huu.hafla hiyo ya makabidhiano yamefanyika ukumbi wa
mikutano wa TFF leo Jumatoano Juni 19, 2013.
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania leo wanakabidhi jezi, vikinga
ugoko, mipira na soksi kwa timu za chini ya umri wa miaka 17
zitakazoshiriki kwenye michuano ya Airtel Raising Stars ngazi za mkoa
ambayo zinatarajiwa kuanza kutimua vumbia kuanzia Juni 23, 2013.
Mikoa
ya kisoka ya Ilala, Temeke na Kinondoni wataingiza timu za wasichana na
wavulana kwenye mashindano hayo huku Mwanza, Morogoro na Mbeya wakileta
timu za wavulana pekee wakati mikoa ya Tanga, Ruvuma na Kigoma
ikishirikisha timu za wasichana tu.
Timu
zote zimeonyesha mwitikio na hamasa kubwa kwa kuwa na maandalizi ya
awali kwa ajili ya kushindana na kushinda katika michuano hiyo. Michuano
ya mikoa itafuatiwa na fainali za taifa ambazo zitapigwa kwenye uwanja
wa Kumbu Kumbu ya Karume jijini Dar es Salaam.
Akiongea
na waandishi wa habari kwenye makabidhiano ya vifaa yailiyofanyika
kwenye ukumbi wa mkutano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) leo,
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando alisema Airtel
wanajivunia kuwa sehemu ya programu ya kuendeleza vijana katika soka la
Tanzania.
“Tunaamini
kuwa ushirikiano wetu na timu ya Manchester United pamoja na TFF
utachangia maendeleo ya mpira wa miguu Tanzania. Tunaimani vijana
wanaweza na ndio maana tunawapa nafasi na kuwasaidia ili waweze kufanya
vizuri zaidi kwenye medani ya soka, “ alisema.
Naye
Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Sunday Kayuni alisema amefurahishwa na
mwitikio ulioonyeshwa na vijana waanaoshiriki kwenye michuano ya Airtel
Raising Stars. “Michuano ya Airtel mwaka huu imekuwa na msisimko mkubwa,
tunawashukuru Airtel kwa kudhamini michuano hii ambayo inatusaidia
kubaini zaidi vipaji vilivyojificha“, alisema Kayuni.
Programu
hii ya Airtel Rising Stars ilimeandaliwa mahsusi kwa vijana wa bara la
Afrika, kwa lengo la vijana wanaochipukia katika soka kuonyesha vipaji
vyao na kupata nafasi kupata mafanikio katika soka.
Katika
kipindi cha miaka miwili iliyopita cha programu hii timu ya Manchester
United walituma walimu wa mpira kwa ajili ya kliniki kwa wachezaji
katika nchi za Tanzania, South Afrika, Gabon na Kenya kwa wachezaji
waliofanya vizuri na kuchaguliwa kwenye michuano hiyo walipata nafasi ya
kufundishwa kusakata kandanda.
Ili
kuwahamasisha vijana, Airtel imeanzisha mashindano ya kimataifa ambayo
mwaka jana yalifanyika kwa mara ya kwanza jijini Nairobi ambapo wavulana
na wasichana walipata fursa ya kuonyesha vipaji vyao. Michuano hiyo
ilishirikisha wachezaji nyota wa ARS kutoka nchi 14 ambazo kampuni hiyo
inafanya biashara.
0 maoni:
Post a Comment