Baada ya siku kadhaa zilizokuwa na kila aina ya harakati, ugumu na
majonzi makubwa, Albert Mangweha aka Ngwair leo amezikwa kwenye makaburi
ya Kihonda mkoani Morogoro ambako ni nyumbani kwao.
/>
Hapa ndipo alipolala Mangweir.
Kabla ya kuzikwa, wananchi wa Morogoro walipata fursa ya kuuaga mwili
wake kwenye uwanja wa Jamhuri. Umati mkubwa wa wananchi ulijitokeza
kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa Ngwair aliyefariki nchini
Afrika Kusini, wiki iliyopita. Wasanii wengi kutoka Dar es Salaam nao
wamehudhuria mazishi hayo.
“Marehemu Albert Mangweha azikwa kishujaa sana ni umati usioelezeka mungu akulaze mahali pema peponi,”
Picha kutoka kwenye akaunti za Instagram za Millard Ayo, Mboni Masimba na Mwasiti. (391)
0 maoni:
Post a Comment