Klabu
ya KITAYOSCE FC imekuwa ya kwanza kutinga katika hatua ya Nusu Fainali ya
Michuano ya Mkombozi Cup 2013 baada ya kuinyuka Nazareth ya Majengo Mjini Moshi
mkoani Kilimanjaro kwa mabao 3-0.
Bao la mapema kabisa la
KITAYOSCE FC lilifungwa katika dakika ya 4 ya mchezo baada ya piga nikupige
langoni mwa Nazareth na kumpa mwanya Festo Antony Kiwale kutupia.
Kipindi cha kwanza
kilimalizika kwa KITAYOSCE FC wakiwa mbele kwa bao 1 kwa bila huku Nazareth wakijutia
nafasi walizozipata na kushindwa kuzitumia.
Katika dakika ya 17 mlinzi
wa kushoto wa Timu ya KITAYOSCE FC
Annuary Mkondo alionekana kutaka kutokana na matatizo ya kifua, ndipo
akaingizwa kiungo Awadhi Gumbo ambaye alienda kubadili nafasi ya Kuingo mkabaji
MeshaCollins alieenda safu ya kulia ya Ulinzi na Petro Mwaipopo akienda
kushoto.
Dakika ya 31 ya mchezo wa
leo uliochezwa katika uwanja wa Mandela katika kata ya Pasua, mjini Moshi Kiungo
wa KITAYOSCE FC Florence Florence alivalia jezi namba 10 ambaye pia ni nahodha
wa klabu hiyo yenye maskani yake katika kata ya Soweto alionyeshwa kadi ya
njano baada ya kumtendea vibaya mchezaji wa Nazareth wakati wakikabana.
Pia katika dakika ya 39
Nazareth walifanya mabadiliko wakimtoa
Mlinzi wa Kati John Mariki aliyeonekana kuchoka na kuingizwa Deo Lyimo
ili kuongeza nguvu.
Hadi dakika 45 za kipindi
cha kwanza zinamalizika KITAYOSCE FC ilikuwa mbele kwa bao moja huku
wakionekana kuchez achini ya kiwango katika kipindi hicho.
Kipindi cha Pili kilianza
kwa mashambulizi makali kwenye lango la Nazareth ambapo Kocha Hamad Haule wa
KITAYOSCE FC alibadilisha mbinu ya kucheza kwa timu yake ambapo ilionekana
kuelewana zaidi.
Mashambulizi hayo yalizaa
matunda kunako dakika ya 58 ambapo Kiungo Florence Florence alipiga shuti la
mbali liliomzidi mlinda mlango wa Nazareth FC Hamidu Khalifa.
Hata hivyo Nazareth
walijitahidi kuweza kuzima wakati mwingine wakijaribu kutoka mbali lakini
walijikuta wakizidiwa na kuishiwa nguvu kabisa kunako dakika ya 72 pale David
Maganga alipofanya kazi ya ziada kwa kuwakimbiza walinzi wa Nazareth na
kumtungua mlinda mlango na kufanya KITAYOSCE FC kuongoza kwa mabao 3-0.
KITAYOSCE FC ilifanya
mabadiliko katika dakika za 79 na 85 kwa kuwatoa viungo Victor Nduzero na Juma
Salehe na kuwaingiza David Brand na Fredrick Temba ambapo mabadiliko hayo
yaliweza kuongeza ladha ya mchezo, uwanjani hapo.
Leo katika Robo Fainali ya
Pili ni Mshindi wa Kundi B ambaye ni Soweto FC atachuana vikali na Golani FC
mechi itakayochezwa katika Uwanja wa King George Memorial.
0 maoni:
Post a Comment