Friday, June 28, 2013

KOMBE LA MABARA:JUMAPILI FAINALI NI BRAZIL v SPAIN

SPAIN_v_ITALY-PENATI_YAOTA_MBAWA

Nusu Fainali ya pili ya Mashindano ya FIFA ya Kombe la Mabara ilikuwa ni patashika ndani ya  Estadio Castelao, Mjini Fortaleza Nchini Brazil kati ya Mabingwa wa Dunia Spain na Italy na kwenda Dakika 90 ngoma ikiwa ngumu kwa Sare ya 0-0 na Dakika 30 za Nyongeza bado ilikuwa 0-0.

Ikaja Mikwaju ya Penati Tano Tano bado ikamalizika 5-5 na ilipokuja Tombola ya Penati za ziada moja moja, Spain waliibuka kidedea kwa kushinda kwa Jumla ya Penati 7-6 baada ya Leonardo Bonucci kupaisha Penati ya 7 ya Italy.

MIKWAJU YA PENATI:
-Wapigaji:
SPAIN 7
-Xavi
-Andres Iniesta
-Gerard Pique
-Sergio Ramos
­-Juan Mata
-Sergio Busquets
-Jesus Navas

ITALY 6
-Antonio Candreva
-Alberto Aquilani
-Daniele De Rossi
-Seb Giovinco
-Andrea Pirlo
-Riccardo Montolivo
­­-Leonardo Bonucci [ALIKOSA-Mpira wapaa!!]

Katika muda mwingi wa Dakika 90 za kawaida, Italy walionekana wako juu lakini watajutia kwa nafasi zao nyingi walizokosa.

Baada ya Dakika 30 za Nyongeza kumalizika, ikaja Mikwaju ya Penati na Beki wa Italy, Leonardo Bonucci, alikosa Penati ya 7 ya Italy kwa kupaisha Mpira juu huku Jesus Navas, alieingizwa toka Benchi, akifunga Penati ya 7 ya Spain na kuwapa ushindi wa Penati 7-6.

Jumapili, Spain watacheza Fainali na Brazil ambao waliwafunga Uruguay 2-1 katika Nusu Fainali nyingine.
Italy na Uruguay zitacheza mapema Jumapili kusaka Mshindi wa Tatu.

VIKOSI:
SPAIN: Casillas, Arbeloa, Sergio Ramos, Pique, Jordi Alba, Xavi, Busquets, Iniesta, Pedro, Torres, Silva
Akiba: Valdes, Albiol, Javi Martinez, Azpilicueta, Villa, Fabregas, Mata, Soldado, Monreal, Cazorla, Jesus Navas, Reina.

ITALY: Buffon, Maggio, Bonucci, Barzagli, Chiellini, Candreva, De Rossi, Pirlo, Marchisio, Giaccherini, Gilardino
Akiba: Sirigu, Astori, De Sciglio, Aquilani, Giovinco, El Shaarawy, Cerci, Montolivo, Diamanti, Marchetti.
Refa: Howard Webb (England)

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU