Sunday, June 9, 2013

REDD'S MISS TANGA, KUSHIRIKI KALEMBO DAY

https://mail-attachment.googleusercontent.com/attachment/u/0/?ui=2&ik=c5efcfe0c1&view=att&th=13f28ed469f5e7c9&attid=0.5&disp=inline&safe=1&zw&saduie=AG9B_P-2CrkZwFZoIv7yIISqZzQc&sadet=1370788450057&sads=j-tSa9uj-XpPEIPk9DLTZ3sDnlk 
https://mail-attachment.googleusercontent.com/attachment/u/0/?ui=2&ik=c5efcfe0c1&view=att&th=13f28ed469f5e7c9&attid=0.7&disp=inline&safe=1&zw&saduie=AG9B_P-2CrkZwFZoIv7yIISqZzQc&sadet=1370788456302&sads=1pja8kHIzLfKJM7gJwg7g3bwMbM
WAREMBO wanaowania shindano la kumtafuta mlimbwende wa mkoa wa Tanga Redd's Miss Tanga 2013 wakiwa katika pozi mara baada ya kumalizika mazoezi yao kwenye ukumbi wa Lavida Loca jijini Tanga,ambapo shindano linatarajiwa kufanyika June 22 mwaka huu katika uwanja wa mkwakwani mjini Tanga.

WAREMBO wanaowania umalkia wa Mkoa wa Tanga “Redd’s Miss Tanga 2013”wanatarajiwa kushiriki katika shughuli za usafi wa mazingira mkoani Tanga “Kalembo Day” June 15 mwaka huu na baadae kutembelea wagonjwa katika hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo kuwaona wagonjwa na kutoa zawadi.
Shughuli hizo za usafi watazifanya katika maeneo mbalimbali jijini Tanga siku hiyo ambayo ni siku maalumu ya usafi katika mkoa wa Tanga wakati wakiwa wanajiandaa na shindano hilo ambalo litafanyika June 22 mwaka huu kwenye uwanja wa Mkwakwani.

Siku mbili baada ya warembo hao kumaliza zoezi hilo watakwenda kutembelea vivutio vya utalii na maeneo ya kihistoria yaliyopo mkoani hapa June 17 mwaka huu lengo likiwa ni kujifunza utalii wa ndani ili kuweza kupata fuksa nzuri ya kuweza kuutangaza kwa wageni na wenyeji.

Vivutio ambavyo warembo hao wanatarajiwa kutembelea ni Mbuga ya Wanyama ya Sadani na Mapango ya kihistoria ya Amboni yaliyopo jijini Tanga ambapo watapata fursa ya kuona na kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu maeneo hayo.
Shindano hilo linatarajiwa kufanyika 22 kwenye Uwanja wa Mkwakwani mkoani hapa ambapo litapambwa na wasanii nguli wa muziki wa bongo fleva nchini ili kuweza kuwapa burudani wakazi wa mkoa huu ambao watajitokeza kushuhudia kinyang’anyiro hicho.

Mkurugezi wa Kampuni ya DATK Intertaimeint, Asha Kigundula, ambaye ndiye muandaaji wa shindano hilo alisema shindano hilo linatakuwa la aina yake kutokana na kuwa na warembo bomba.

Alisema kuwa warembo hao tayari wanaedelea na mazoezi kwenye Ukumbi wa Lavida uliopo jijini Tanga ambapo tayari wameshaanza kuwateka wadau wa tasnia hiyo ambao wamekuwa wakijitokeza kila siku kushuhudia mazoezi hayo.

   “Ninachoweza kusema shindano la mwaka huu litakuwa la aina yake kutokana na kusheheni warembo bomba wenye mvuto na hivyo kuonyesha kutakuwa na mchuano mkali miongoni mwao “Alisema Kigundula

Shindano hilo litaanza saa 2, usiku na kueleza kuwa maandalizi ya shindano hilo yanaendelea vizuri na jumla ya warembo 12 watashindania taji hilo ambalo hivi sasa linashikiliwa na Miss Tanga 2012 Teresia Kimolo.

Warembo hao ni Hawa Ramadhan (18),Hazina Mbaga (19)Like Abdulraman (19), Jack Emannuel (18),Wahida Hashimu(20), Tatu Athumani (19), Mwanahamis Mashaka(20), Neema Abdallah (18), Winfrida Gutram (21)Lulu Mbonea (19) na Aisha Rashid (21),Azina Daniel (19),Lulu Matawalo(22),Judithi Moreli (21) na Hawa Twaybu(21)

Alisema kwamba shindano la mwaka huu litaandika historia mpya ya urembo mkoani humo kwa kuwa Kampuni DATK imejipanga, hivyo mashabiki wa mashindano ya urembo wa jijini hapo kwa ujumla wakae mkao wa kupata raha.

Redd's, Miss Tanga, imedhaminiwa na Dodoma Wine,CXC Africa,Executive Solutions,Busta General Supply, Mkwabi Interprises,Lusindic Investment LTD, Lavida Pub,Jambo Leo,Staa Spoti,Five Brothers Cloud's Media Group,  pamoja na Blog Michuzi Media Group,Bongostaz.com, Saluti5,Kajuna, JaneJohn, na Kidevu na assengaoscar.blogspot.com.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU