Mkuu wa
Wilaya ya Arusha, John Mongella ( kushoto) akimkabidhi mjasiliamali,Joyce Mmali
Mashine ya kusaga wakati wa hafla ya
kukabidhi ruzuku za wajasiliwamali wa Safari Lager Wezeshwa kanda ya Kaskazini ilifanyika katika viwanja
vya General Tyre Arusha mwishoni mwa wiki.Kulia ni Meneja wa Bia ya Safari
Lager, Oscar Shelukindo na Meneja mauzo wa Kanda ya Kaskazini, Wilderson Kitio.
Mjasiliamali,Judith
Tarimo(kushoto) akiangalia zawadi yake mara baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa
Wilaya ya Arusha, John Mongella(wa pili kulia) wakati wa hafla ya kukabidhi
ruzuku za wajasiliwamali wa Safari Lager Wezeshwa kanda ya Kaskazini ilifanyika katika viwanja
vya General Tyre Arusha mwishoni mwa wiki.Kulia ni Meneja wa Bia ya Safari
Lager, Oscar Shelukindo.
Mkuu wa
Wilaya ya Arusha, John Mongella (wa pili kushoto) akimkabidhi
mjasiliamali,Veronica Tarimo Mashine ya kusaga
vyakula vya kuku wakati wa hafla ya kukabidhi ruzuku za wajasiliwamali
wa Safari Lager Wezeshwa kanda ya
Kaskazini ilifanyika katika viwanja vya General Tyre Arusha mwishoni mwa
wiki.Kulia ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo na Meneja mauzo
wa Kanda ya Kaskazini, Wilderson Kitio.
MKUU wa
Wilaya ya Arusha,John Mongella amewakabidhi ruzuku wajasiliamali 10 wa Kanda ya
Kaskazini zilinazotolewa na Kampuni ya Bia Tanzania kupitia Bia ya Safari Lager
inayoendesha program inayoitwa Safari Lager Wezeshwa.
Akizungumza
na wajasiliamali pamoja na wakazi wa arusha walijitokeza kushuhudia tukio hilo
ikiwa na kupata burudani aliwataka wajasiliama wakavitumie vitendea kazi hivyo
walivyopewa viwasaidie kuinua maisha yao na jamii inayowazunguka ifaidike
ambapo hata serikali itafaidika pia kama adhima ya safari lager na si kuviweka
ndani.
Mongella
aliwataka wajasiliama wakawe mfano wa kuigwa katika jamii kwa ruzuku walizopewa
na wakawe mabalozi wazuri kwa kuitangaza Safari Lager ikiwa ni pamoja na kinywa
ukizingatia ndio Bia namba moja Afrika kwa sasa.
Mkuu wa
Wilaya huyo pia aliipongeza TBL kupitia Bia ya Safari Lager kwa kuanzisha
program hiyo ya kuwawezesha wajasiliamali na kuwaomba isiishie mwaka huu bali
iwe endelevu na akasema serikari inatambua mchango wao na mahala watakapo kwama
iko tayari kusaidia.
Nae Meneja
wa Bia ya Safari Lager Oscar Shelukindo aliwakumbusha wajasiliamali pamoja na
semina waliyopewa ya namna ya kuendesha biashara lakini lengo kuu la ruzuku
hizo ni kukunufaisha wewe mjasiliamali,familia yako na jamii inayokuzunguka
hivyo aliwaomba wakafanye hivyo na si kuvifungia ndani vifaa walivyopewa.
Shelukindo
alisema yuko tayari kumsaidia mjasiliamali alipiga hatua kwa kumuongezea kitu
alichokwama ili apige hatua zaidi ya maendeleo.
Programu ya
Safrai Lager Wezeshwa ilianza mwaka juzi na hili ni mara ya pili kutoa ruzuku
kwa wajasiliamali .Mwaka jana Safari Lager ilitoa milioni 200 kwa wajasiliamali
57 kwa nchi nzima ya Tanzaina na Mwaka huu imetoa tena milini 200 ambapo
wajasiliamali 47 wanawezeshwa natayari Kanda ya Pwani na Dares Salaam
wameshakabidhiwa na mwishoni mwa wiki Mkuu wa Wilaya ya Arusha, John Mongella
amewakabidhi wajasiliamali wa Kanda ya Kaskazini na wiki ijayo ni Kanda ya Ziwa
ambapo hafla ya kukabidhi itafanyika jijini Mwanza.
0 maoni:
Post a Comment