Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Bi Anna
Rose Nyamubi(kushoto) akikabidhi zawadi kiongozi wa kundi la Ngoma la Mabulo ya Jeshi shilingi
laki tano mara baada ya kushika nafasi ya pili katika mashindano ya Balimi
Ngoma Mkoa wa Shinyanga yaliyomalizika mwishoni mwa wiki.Kushoto ni Meneja
Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Mkoa wa Shinyanga, Robert Kazinza na
Meneja matukio TBL Kanda ya Ziwa, Erick Mwayela.
Kiongozi wa kundi laNgoma la Wagoyangi,
Ngelela Ng'wanajiluguja(katikati) akifurahia kitita cha shilingi laki sita mara
baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga,Annarose Nyamubi(wa pili
kushoto) mara baada ya kuibuka mabingwa katika mashindano ya Ngoma Mkoa wa
Shinyanga yanayodhaminiwa na Bia ya Balimi,yaliyomalizika mwishoni mwa wiki
Mkoani humo.Kushoto ni Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Mkoa wa
Shinyanga, Robert Kazinza na Meneja matukio TBL Kanda ya Ziwa, Erick Mwayela.
KUNDI la Ngoma la Mwanajilunguja
limefanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya Ngoma Mkoa wa Shinyanga
yanayodhamniwa na Kampuni ya Bia Tanzania kupitia kinywaji Balimi Extra Lager
yaliyomalizika mwishoni mwa wiki mkoani humo.
Kundi la Mwanajilunguja lilitwaa
ubingwa huo kwa alama 82,na kuzawadiwa fedha taslimu Sh.600,000/= na tiketi ya
kuwakilisha Mkoa wa Shinyanga katika fainali za mashindano ya Kanda
yanayotarajiwa kufanyika Julai 20 mwaka huu jijini Mwanza.
Washindi wa pili katika mashindano
hayo ni kundi la Mabulo ya Jeshi ambao walipata alama 80 hivyo kujinyakulia
fedha taslimu Sh.500,000/=,nafasi ya tatu ilichukuliwa na kundi la Wagoyangi
Usule kwa alama 79 na kuzawadiwa Sh.400,000/=,nafasi ya nne ilichukuliwa na
Wagoyangi Bugimbagu kwa alama 73 ambao walizawadiwa Sh.400,000/=
Jumla ya vikundi vilivyoshiriki
mashindano ya Ngoma Mkoa wa Shinganga ni
10,ambapo vikundi shiriki 6,vingine vilipewa kifuta jasho cha fedha taslimu
Sh.150,000/= kila kikundi.
Akizungumza na washiriki wa
mashindano hayo pamoja na wakazi wa Shinyanga waliojitokeza kushuhudia fainali
hizo, Mkuu wa Wilaya ,Annarose Nyamubi aliwapongeza washiriki wote kwa ushiriki
wao katika mashindano hayo na pia kwa kuendeleza mila na desturi za ngoma za
asili lakini zaidi aliipongeza Kampuni ya Bia Tanzania kupitia Bia ya
Balimi Extra Lager ambao wanadhamini
mashindano hayo kwa kujua udhamani wa Ngoma za asili.
Mkuu huyo wa wilaya amesema kuwa kwa
kutumia mashindano kama hayo jamii imekuwa ikiburudika na kutukumbusha
tamaduni zetu ambazo mara nyingi zimekuwa zikisahaulika kwa wengi na kuiomba
kampuni ya TBL kuendelea kudhamini mashindano hayo na kuwataka kutosita
kushilikiana na serikali katika masuala mbalimbali ya kijamii kwa kuwa kwa
kufanya hivyo wamekuwa wakisaidia baadhi ya majukumu ya serikali.
Aidha mkuu huyo wa wilaya amevitaka
vikundi hivyo kuzitumia fedha wanazo zipata katika kujiletea maendeleo ikiwemo
kuanzianzisha vikundi vya kuweka na kukopa ili viweze kuwasaidia katika
kuwalete maendeleo.
Naye Meneja wa Kampuni ya bia
Tanzani (TBL) Robert Kazinza amesema kuwa kampuni yake imekuwa ikishiriki
katika kudhamini shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo michezo na
burudani ikiwa ni shukrani zao kwa jamii kwa kutumia bidhaa zao ambapo ameiomba
jamii ili kampuni hiyo iweze kuendelea kudhamini shughuli hizo wawaunge mkono
kwa kutumia bidhaa zao, hasa bia ya Balimi Extra Lager bia ya Kanda ya Ziwa
pekee.
Vikundi vingine ambavyo vimeshiriki
katika fainali hizo ni pamoja na Buzoli Ngunga, Kadete, Wagoyangi Maswa,
Waulinguli Bugimbagu, Bugali na Shinyanga Art Group, fainali hizo zitaendelea
wiki ijayo ili kumpata mshindi wa fainali hizo katika mkoa wa Kagera, ambaye
ataungana na washindi wengine ambao watashiriki mashindano hayo ngazi ya kanda
yatakayo fanyika jijini Mwanza Hivi karibuni.
0 maoni:
Post a Comment