Chama
cha Waamuzi mkoa wa Kilimanjaro kimegoma kuwatumia waamuzi wake katika Michuano
ya Mkombozi Cup inayoendelea katika Mji wa Moshi kwa kile kinachodaiwa malipo
madogo, kudharauliwa na kuburuzwa na Kamati ya Michuano husika.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kamati
ya Mkombozi Cup 2013 kwa vyombo vya habari mchana wa leo imesema waamuzi
waliokuwa wakiwatumia ni kutoka FRAT mkoa wa Kilimanjaro ambao wamegomea kuendelea
na kuchezesha mechi zilizobaki.
Hatua hiyo imekuja wakati ikiwa
ni siku 4 tu baada ya michauno hiyo kuanza kutimua vumbi katika Viwanja vya
Shule ya Msingi Mandela(PASUA) na King George Memorial (SOWETO).
Sehemu ya Taarifa hiyo imesema
kuwa mechi zilizokuwa zichezwe leo katika viwanja hivyo zimeahirishwa mpaka
kesho Jumanne ya Juni 18, 2013.
Mechi hizo ni Nazareth dhidi ya
Soweto katika uwanja wa Memorial (KUNDI B) na Best Maridadi dhidi ya Moshi
United katika uwanja wa Mandela (KUNDI C).
Hata hivyo Kamati ya kuendesha
michuano hiyo imesema inaendelea kutafuta waamuzi kutoka sehemu nyingine kwa
ajili ya michuano hiyo.
JAIZMELALEO
imefuatilia kwa kina na kutaka kujua mwaka ujao Mkombozi Cup 2014 itaweza kuwatumiwa waamuzi kutoka katika Mkoa
wa Kilimanjaro na kwamba itawatumia waamuzi kutoka katika Wilaya ya Moshi pekee
ili kuweza kukidhi uwezo wao.
Aidha imebainika kwamba waamuzi
wa mchezo wa soka hawapatani wao kwa wao kiasi kwamba hakuna maelewana kati ya
uongozi na waamuzi wenyewe.
MKOMBOZI CUP 2013
|
||||
KUNDI A
|
KUNDI B
|
KUNDI C
|
KUNDI D
|
|
1
|
KITAYOSCE
|
KILI RANGERS
|
TPC
|
RELI
|
2
|
GREEN STAR
|
MVULENI
|
NEW GENERATION
|
SANGO
|
3
|
NYUKI FC
|
NAZARETI
|
BEST MARIDADI
|
KILI FC
|
4
|
GOLANI FC
|
SOWETO FC
|
MOSHI UTP
|
BOYS UTD
|
0 maoni:
Post a Comment