Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana
na Mlezi wa Tamasha la asili la Watu wa Mangapwani,
Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya
Tamasha hilo, Mwinyi Jamari Ramadhan Nasib, pamoja na baadhi ya viongozi wakati akiwasili kwenye viwanja vya Mangapwani jana Juni 15, 2013 kwa ajili ya kufunga rasmi Tamasha hilo
lililoanza Juni 14.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia bidhaa zinazotengezwa na vikundi vya akina
mama wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonyesho katika Tamasha
la Asili la Watu wa Mangapwani, alipofika kufunga rsmo tamasha hilo jana Juni 15, 2013, mjini Munguja.
Katika Tamasha hilo kulikuwa na mashindano ya michezo mbalimbali ya asili,
kama Bao la Kete, Kufua Nazi, na kama mchezo huu pichani
vijana wakishindana kukwea Minazi, ambapo kwa upande wa michezo Tamasha
hilo lilihitimishwa kwa mchezo wa fainali ya Soka.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana
na Mlezi wa Tamasha la asili la Watu wa Mangapwani,
Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya
Tamasha hilo, Mwinyi Jamari Ramadhan Nasib, pamoja na baadhi ya viongozi, kwa pamoja wakifurahia mchezo wa kukwea
minazi wakati wa Tamasha hilo.
Baadhi ya washiriki wa mchezo wa kufua Nazi, wakichuana kufua Nazi hizo ambapo kila mmoja alitengewa jumla ya Nazi 20, na mchezaji wa kwanza (kushoto) ndiye aliibuka mshindi kwa kuwaacha wenzake na Nazi nyingi zaidi wakiendelea kuchuana wawili.
Wasanii wa Kikundi
cha Sanaa na michezo ya asili cha Luperwa Zanzibar Group, chenye maskani
yake Bububu, wakitoa burudani wakati wa hafla ya kufunga Tamasha hilo,
lililofungwa na Mhe. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt. Mohammed Gharib Bilal, jana Juni 15, 2013 Mangapwani.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifunga
mlango wa Kibanda cha Makuti kama ishala ya kufunga
rasmi Tamasha hilo la Watu wa Mangapwani, jana Juni 15, 2013,
lililofunguliwa na Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, Juni 14. Picha na OMR
0 maoni:
Post a Comment