Monday, June 17, 2013

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ATEMBELEA KISIMA CHA CHINI YA ARDHI CHA MANGAPWANI UNGUJA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja na msimamizi wa Kisima cha Chini kwa Chini, Abdulwakir Zahro, wakati alipofika kutembelea na kujionea Kisima hicho cha Chini kwa Chini, kilichopo Mangapwani, Wilaya ya Kaskazini B, Mkoa wa Kaskazini Unguja jana Juni 15, 2013. Kushoto ni Mlezi wa Tamasha la Asili la watu wa Mangapwani, Ali Hassan Mwinyi.
 Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiingia shimoni wakati alipofika Mangapwani Kutembelea na kujionea Kisima cha Chini kwa Chini, kilichokuwa kikitumiwa na Wakoloni kupitishia Watumwa. Kisima hicho kilicho chini ya Ardhi huko ndani kuna Njia tatu, mbili zinatokezea Baharini na moja inatokezea katika moja ya Kijiji cha Mangapwani, ambayo hadi leo haijajulikana mwisho wa njia hiyo inapotokezea
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoka shimoni kuangalia Kisima cha chini kwa chini kilichopo Mangapwani, ambacho kilikuwa kikitumiwa na Wakoloni kupitishia Watumwa. Kisima hicho kilicho chini ya Ardhi ndani kuna Njia tatu, mbili zinatokezea Baharini na moja inatokezea katika moja ya Kijiji cha Mangapwani, ambayo hadi leo haijajulikana mwisho wa njia hiyo inapotokezea. Picha na OMR

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU