Katibu
Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam,Edward Otieno(kulia) akimkabidhi mjasilamali,Pinie Mwasha mashine
ya maabara(Outclave sterilizer) wakati wa zoezi la kukabidhi vifaa vya ruzuku
kwa wajasiliamali waliofuzu kwenye program ya Safari Lager Wezeshwa kwa kanda
ya Pwani iliyofanyika katika Viwanja vya Leaders Dar es Salaam mwishoni mwa
wiki.Katikati ni Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscar Shelukindo.
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam,Edward Otieno(kulia) akimkabidhi mjasilamali,Jamhuri Oiso mashine
ya kutengeneza soli za viatu wakati wa zoezi la kukabidhi vifaa vya ruzuku kwa
wajasiliamali waliofuzu kwenye program ya Safari Lager Wezeshwa kwa kanda ya
Pwani iliyofanyika katika Viwanja vya Leaders Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
WANAWAKE nchini wameshauriwa kujenga tabia ya kujitokeza kwa wingi
kushiriki shughuli za kijamii ambazo zinaweza kuwainua kimaendeleo.
Ushauri huo ulitolewa juzi na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Edward Otione wakati alipomwakilisha Mkuu wa Mkoa huo, Said Meck Sadick katika hafla ya kukabidhi ruzuku za vitendea kazi kwa wajasiriamali 13 kutoka mikoa ya Pwani, Lindi, Mtwara na Dar es salaam.
Ushauri huo ulitolewa juzi na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Edward Otione wakati alipomwakilisha Mkuu wa Mkoa huo, Said Meck Sadick katika hafla ya kukabidhi ruzuku za vitendea kazi kwa wajasiriamali 13 kutoka mikoa ya Pwani, Lindi, Mtwara na Dar es salaam.
Hafla ya kuwakabidhi ruzuku za vitendea kazi kwa wajasiriamali hao ambao ni sehemu ya wajasirimali 46 kutoka mikoa 23 waliofanikiwa kushinda katika zoezi la mpango wa 'Safari Lager Wezeshwa', ilifanyikia kwene viwanja vya Leaders Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Otione alisema kuwa wanawake wamekuwa waoga kujitokeza kushiriki kwenye shughuli mbalimbali za kijamii kwa kujiona kama hawawezi wakati wanaweza endapo watawezeshwa.
"Nimefurahia kusikia kwamba kati ya wajasiriamali 46 watakaowezeshwa ruzuku za vitendea kazi vya kuinua biashara zao mwaka huu, wanawake ni 27, hivyo nawapongeze kwa kujitokeza kushiriki katika mpango huu wenye manufaa ya kuwainua wajasirimali wadogo wadogo nchini na niwaombe wanawake wengine zaidi wasisite kujitokeza kushiriki katika shughuli yoyote ya kijamii kwani wakiwezeshwa wanaweza,"alisema Otione.
Aliongeza kwa kuwataka wajasirimali wanaowezeshwa katika mpango huo kutumia vizuri ruzuku wanazowezeshwa ili ziweze kuwanufaisha wao pamoja na jamii iliyowazunguka.
"Pia niwapongeze wadhamini wa mpango huu bia ya Safari Lager kwa kwa kuanzisha mpango huo ambao lengo lake ni zuri katika kupambana na umasikini nchini na serikali inatambua mchango wenu huo na kwa kuwa nisikia ni mpango endelevu endeleeni nao ili kuwainua wafanyabiashara wadogo wadogo,"alisema.
Naye meneja wa bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo alisema kuwa mara baada ya kumaliza kutoa ruzuku kwa wajasiriamali wote 46 walioshinda kuwezeshwa ruzuku katika mpango huo, zoezi la utoaji fomu kwa ajili ya mpango huo kwa mwaka huu litaanza mara moja.
"Hawa wajasirimali ambao tumeanza kuwapa ruzuku zao leo ni wa mwaka jana, hivyo tukimaliza kutoa ruzuku kwa wajasirimali wote, zoezi la utoaji fomu kwa ajili ya mpango huo mwaka huu litaanza mara moja, hivyo wajasiriamali wadogo wenye nia ya dhati ya kutaka kuwezeshwa ruzuku za kukuza biashara zao ili ziwasadie wao na jamii iliyowazunguka wajiandae kwa zoezi hilo, "alisema Shelukindo.
0 maoni:
Post a Comment