Friday, July 12, 2013

AIRTEL YATOA FUTARI KWA WATOTO YATIMA MIKOA MINNE

 Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye hafla fupi ya makabidhiano  ya vyakula vya kufuturisha watoto yatima katika vitu vilivyopo mikoa ya Dar es salaam, Mbeya, Arusha, Mwanza katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani iliyofanyika  katika ofisi za Airtel jijini Dar Es Salam ,akifuatiwa na meneja wa huduma za Jamii wa Airtel bi Hawa Bayumi.
 Meneja  Uhusiano wa Jamii wa Airtel bi Hawa Bayumi  akimkabidhi mwakilishi wa Bakwata Ustadh Hassan Malangali vyakula vya kufuturisha katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani  vilivyotolewa kwa vituo vitatu  vya watoto yatima Dar es Salaam (hawapo pichani)  vituo vitakavyofaidika zaidi ni vya Dar es salaam, Mbeya, Mwanza, Arusha hafla ya makabidhiano iliyofanyika  katika ofisi za Airtel  Morocco jijini Dar Es Salam .
 Meneja  Uhusiano wa Jamii wa Airtel bi Hawa Bayumi  akiwakabidhi Saida Makope mmoja wa wakilishi wa kituo cha watoto yatima mjini Dar Es Salaam  katika  hafla fupi ya makabidhiano  ya vyakula vya kufuturisha katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani  vilivyotolewa kwa vituo vitatu vya watoto yatima jijini Dar Es Salaam  iliyofanyika katika ofisi za Airtel  Morocco jijini Dar Es Salam  akifuatiwa na mwakilishi wa Bakwata ustadhi Ustadh Hassan Malangali .
 Wateja Airtel sasa kupata muda wa dua, nukuu za qurani, mawaidha kwa kutuma neno Ramadhani kwenda 15322 kwa shilingi 153 tu kwa siku.
Kampuni za simu za mkononi za Airtel Tanzania kupitia Kitengo chake cha huduma kwa Jamii wametoa msaada kwa vituo vitatu jijini Dar Es Salaam vya watoto yatima katika mwezi mtukufu wa Ramadhani vikifuatiwa na vituo vingine katika mikoa ya Arusha, Mwanza na Mbeya ili kusaidia watoto wanaolelewa kwenye vituo hivyo.

Msaada huo umetolewa kwa lengo la kuwalenga watoto kutoka mikoa minne ambayo ni Dar Es Salaam, Arusha, Mwanza na Mbeya kwa watoto hawa wanaohitaji upendo  hususani katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani. Baadhi ya vitu vilivyotolewa ni Mchele,Sukari, maharagwe,unga, mafuta ya kupikia,maziwa, juice, majani ya chai na sabuni vyenye dhamani ya shilingi milioni tano na nusu.

Akizungumza katika hafla hiyo ya makabidhiano iliyoandaliwa katika makao makuu ya  Airtel jijini Dar Es Salaam, Meneja uhusiano wa huduma kwa Jamii bi Hawa Bayumi alisema "kwa kutambua umuhimu wa Jamii tunayofanya nayo biashara kampuni ya Airtel tumeamua turudishe kiasi cha faida tunayopata kwa wananchi ili iwasaidie.

Akifafanua alisema kwa muda wa miaka 11 iliyopita tumeweza kusaidia Jamii mbalimbali ya watanzania ndani ya mfungo wa Ramadhani na bila kuacha nyanja za elimu, michezo kwa watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu na kukosa huduma mbalimbali za kijamii.

Kwa mwaka huu kupitia Kitengo chake cha huduma kwa Jamii tutarudisha tulichokipata na tutaweza kufikia watoto zaidi ya 300 wa mikoa ya Dar Es Salaam, Arusha , Mwanza na Mbeya na mpaka sasa  kwa mwaka huu Airtel imegharamia zaidi ya shilingi millini 150 katika kukuza kiwango  cha elimu kwa watoto wetu hapa Tanzania," alisema Bayumi.

Bayumi aliongeza kwa kusema kwamba Airtel inapenda kuwatakia kheri na Baraka katika mwezi huu mtukufu na tangu kuanza kwa Mwezi mtukufu wa Ramadhan, wateja wa Airtel wanaweza kufurahia huduma maalumu ya  Ramadhani kwa kutuma neno RAMADHANI kwenda namba 15322 kwa shilingi 153 tu kwa siku. Katika huduma hii mteja atapokea dua, nukuu za qurani, mawaidha na taraweh salat moja kwa moja kwenye simu yake, kila siku.

Naye katibu mkuu wa Bakwata Sheikh Suleiman Lolila  ambaye alikuwa mgeni rasmi alisema mbali ya hafla hiyo makabidhiano ya chakula imetoa fursa kwa waislam kutoka maeneo mbalimbali kukutana pamoja na kukumbushana juu ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Aidha Lolila licha ya kuishukuru Airtel Tanzania kwa misaada inayotoa kwa Jamii alisema jambo hilo linahitaji pongezi na kutaka liungwe mkono na kuigwa na kampuni zingine hapa nchini.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU