Wednesday, July 24, 2013

BancABC YAJUMUIKA NA WATEJA WAKE KUPATA

 Mgeni rasmi wa hafla futari iliyoandaliwa na Benki ya BancABC kwa wafanyakazi wa makampuni mbalimbali, Sheikh Ismail Mohamed Salim akizungumza na wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa hafla hiyo iliyofanyika katika Hotel Kempisk Kilimanjaro mwishoni mwa wiki.
Meneja wa Benki ya BancABC wa kitengo cha huduma za kibenki kwa makampuni na taasisi Bwana Zulfikar Chandoo akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Kempisk Kilimanjaro mwishoni mwa wiki.
Wageni waalikwa wakipata futari
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akifuturu wakati wa hafla hiyo

BENKI ya BancABC leo hii imeandaa hafla fupi kujumuika kwa pamoja na wateja wake waliofunga katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani ili kupata futari. Hafla hii fupi imefanyika jijini Dar Es Salaam katika hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro na imehudhuriwa pia na Sheikh Ismail Mohamed Salim ambaye alikuwa mgeni wa rasmi.
Akizungumza katika hafla hii Meneja wa Benki ya BancABC wa kitengo cha huduma za kibenki kwa makampuni na taasisi Bwana Zulfikar Chandoo alisema kwamba, “BancABC tunathamini mchango mkubwa tunaopata kutoka kwa wateja wetu na tumeandaa hafla hii fupi ili kujumuika nanyi jioni hii ya leo ili kupata futari. Kwa kupitia mkusanyiko kama huu, tunadumisha mahusiano yetu ya kibiashara, tunajiweka karibu zaidi na marafiki, jamaa na ndugu zetu bila kujali tofauti zetu za kiutamaduni, imani au kidini”.

Mgeni rasmi wa hafla hii Sheikh Ismail Mohamed Salim aliwapongeza sana benki ya  BancABCkwa kutambua mchango wa wateja wake wanaofunga na kujitolea kuandaa shughuli hii. Aliwaasa waislamu kumkumbuka Mungu katika shughuli zao za kila siku kwani huo ndio mwanzo wa mafanikio katika biashara na shughuli nyinginezo za binadamu. Aliongeza pia, “ Tukio kama hili la Futari, linatupa nafasi ya kuungana na kutambua mchango muhimu ambao jumuiya ya kiislamu umetoa kwenye Historia na Urithi wa nchi yetu nzuri ya Tanzania.

Bwana Zulfikar alimalizia kwa kusema, “Tunapenda kuwashukuru wateja wetu wote kwa kuchagua BancABC, tunapenda pia kuwakumbusha wateja wetu watakaosafiri kwenda Macca kwa ajili ya Hijja mji wa Mecca mwezi October mwaka huu, wafike kwenye ofisi zetu ili wajipatie kadi za VISA za kusafiria. Kadi hii ni njia salama na kusafiri na fedha zako popote uendapo. Unaweza kujipatia aidha kadi ya malipo ya kabla ya BancABC VISA cash card au kadi maalumu za kusafiria za BancABC VISA Travel Money. Kadi hizi ndio njia salama na rahisi ya kubeba fedha pale mtu anaposafiri nje ya nchi na dunia nzima kwa ujumla”. Aliongezea kuwa, BancABC ina huduma kabambe ya Kutoa mikopo wa Wajasiriamali kwa vigezo nafuu zaidi, ambapo wafanya biashara wadogowadogo wanaweza kujipatia mikopo ya kukuza biashara zao haraka na kwa urahisi zaidi kwani mfanyabiashara haitaji kuweka dhamana yoyote ili kupata mkopo huo. Tafadhali fika kwenye moja kati ya matawi yetu ya BancABC yaliyopo Dar es Salaam na Arusha ili upate maelezo zaidi na uanze kunufaika na huduma za BancABC.
Baadhi ya Wafanyakazi wa BancABC wakipata futari wakati wa hafla hiyo

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU