Wednesday, July 24, 2013

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA MABADILIKO YA TABIANCHI, CHANGAMOTO ZA MAENDELEO NA UKUAJI WA MIJI BARANI AFRIKA, JIJINI ARUSHA LEO

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa kuhusu mabadiliko ya Tabianchi, Chanagamoto za Maendeleo na ukuaji wa Miji Barani Afrika. Mkutano huo umefunguliwa leo Julai 24, 2013 Jijini Arusha.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya Jarida la Sayansi, kutoka kwa Mkurugenzi wa Sayansi 'Physical Sciences' (COSTECH) Prof. Clavery Tungaraza, baada ya Makamu kufungua rasmi mkutano huo uliofanyika kwenye Hoteli ya Mount Meru, Jijini Arusha leo Julai 24, 2013.
 Profesa Rwekaza Mukangara, akizungumza kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais kufungua mkutano huo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na na baadhi ya washiriki wa mkutano huo baada ya ufunguzi rasmi.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais wakati akisoma hotuba yake ya ufunguzi. Picha na OMR

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU