JAJI
Steven Ihema na wakili mwandamizi, Bi. Jesse Mguto wataongoza kamati
muhimu za za maadili za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
zilizoundwa baada ya kufanya mabadiliko kwenye katiba ya Shirikisho hilo
mwishoni mwa wiki iliyopita, Rais wa TFF Leodegar C. Tenga alitangaza
jana.
Shirikisho
hilo pia limemteua Jaji Bernard Luanda kuongoza Kamati ya Rufaa za
Uchaguzi wakati Profesa Mgongo Fimbo ataendelea kuongoza Kamati ya Rufaa
za Nidhamu na Kamanda Mstaafu, Alfred Tibaigana akiendelea kuwa
mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu.
Rais
Tenga alisema hayo wakati alipoongea na waandishi wa habari jana kwenye
ukumbi wa mikutano wa Uwanja wa Taifa mara baada ya kumalizika kwa kikao
cha Kamati ya Utendaji, ambacho kikatiba kina jukumu la kuunda Kamati
Ndogo za TFF na vyombo vya maamuzi.
“Tulitaka
tuwe na watu solid (imara) na makini ambao watatuhakikishia tunakwenda
vyema,” alisema Tenga akizungumzia uteuzi huo ambao unahitimisha
mchakato wa mageuzi kwenye Shirikisho baada ya Uchaguzi Mkuu wa TFF
uliopangwa kufanyika mwezi Februari kusimamishwa kutokana na baadhi ya
wagombea kupinga kuenguliwa na baadaye kwenda FIFA.
Katika
kumaliza tatizo hilo, FIFA ilituma ujumbe wake kusikiliza walalamikaji
na watu wengine na baadaye kuagiza kuundwa kwa Kamati za Maadili na
kufanyika kwa Mkutano Mkuu Maalum wa TFF kwa ajili ya kuingiza vyombo
hivyo kwenye katiba kabla ya kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa TFF.
“Tumezingatia
pia maoni ya wajumbe wa Mkutano Mkuu ambao walitaka kamati ziwe na
majaji... lakini si rahisi kupata seating judges (majaji walio kazini)
ndio maana tunawashukuru wale waliotuambia kuwa wako tayari kutusaidia.
“Tumetafuta
majaji na mawakili waandamizi ambao tunaamini watatuhakikishia haki
inatendeka na inaonekana inatendeka,” alisema Tenga na kuongeza kuwa pia
walizingatia maombi ya wajumbe wengine watatu ambao walitaka kupumzika,
akiwataja kuwa ni Deo Lyatto, Sylvester Faya na Idd Mtiginjollah.
Alisema
kutokana na mfumo huo mpya, mambo yote yanayohusu masuala ya ndani ya
uwanja sasa yatashughulikiwa na Kamati ya Nidhamu, wakati yale ya nje ya
uwanja, ambayo yanawahusu viongozi na wanafamilia ya mpira wa miguu kwa
ujumla, yatashughulikiwa na Kamati za Maadili.
Tenga
alisema mabadiliko hayo pia yamegusa kamati nyingine mbili, yaani Kamati
ya Nidhamu na Kamati ya Uchaguzi ambayo sasa itaongozwa na Mwanasheria
Mkuu wa zamani wa Zanzibar, Hamidu Mbwezeleni
Jaji
Ihema ataongoza Kamati ya Rufaa za Maadili akisaidiwa na mwanasheria
mwingine mwandamizi, Victoria Makani, huku Bi. Mguto, ambaye anakuwa
mwanamke wa kwanza kuongoza vyombo vya vya maamuzi ataongoza Kamati ya
Maadili akisaidiwa na makamu wake Francis Kabwe, ambaye Msajili wa
Mahakama Kuu.
Katika
uteuzi huo, baadhi ya wajumbe wamehamishwa kutoka kamati moja hadi
nyingine. Mhe. Murtaza Mangungu, ambaye awali alikuwa Kamati ya Rufaa za
Uchaguzi, sasa ataingia kwenye Kamati ya Rufaa za Maadili; Kamanda
Mohamed Mpinga na Prof Madundo Mtambo wamehamishwa kutoka Kamati ya
Rufaa za Uchaguzi kwenda Kamati ya Maadili.
Wajumbe
wapya kwenye Kamati hizo ni pamoja na kocha wa zamani wa Taifa Stars na
Reli ya Morogoro, Mshindo Msolla na Kamanda Mstaafu Jamal Rwambow
wanaingia kwenye Kamati ya Nidhamu; mwanasheria maarufu Evodi Mmanda
anaingia kwenye Kamati ya Maadili; mwanasheria mwandamizi Mustapha
Kambona ambaye anaingia kwenye Kamati ya Nidhamu; Mhe. Mohamed Misanga
ambaye anaingia kwenye Kamati ya Maadili na Kanali Iddi Kipingu, ambaye
anasifika kwa kuendesha soka la vijana, anaingia kwenye Kamati ya Rufaa
za Nidhamu.
Pia
Mwanasheria Anne Steven Marealle anakuwa mjumbe kwenye Kamati ya Rufaa
za Uchaguzi; Yohane Masale (Rufaa za Uchaguzi), Allen Kasamala (Rufaa za
Uchaguzi); Francis Kiwanga ambaye pia aningia kwenye
Kamati ya Rufaa za Uchaguzi na mkufunzi wa FIFA, Henry Tandau ambaye
anaingia kwenye Kamati ya Rufaa za Maadili.
Kamati ya
Utendaji pia imefanya mabadiliko kwenye Kamati ya Waamuzi ambako
mwenyekiti Said Nassoro na katibu Charles Ndagala wa Chama cha Waamuzi
wanaingia kwenye kamati hiyo kushika nafasi ya Joan Minja na Riziki
Majala.
Wajumbe wa Kamati hizo ni kama ifuatavyo:
Kamati ya
Rufaa za Maadili ni Jaji Steven Ihema (mwenyekiti), Victoria Makani
(m/mwenyekiti), Mhe. Mohamed Misanga, Henry Tandau na Mhe. Murtaza
Mangungu.
Kamati ya
Maadili: Bi Jesse Mguto (mwenyekiti), Francis Kabwe (m/mwenyekiti), ACP
Mohamed Mpinga, Prof. Madundo Mtambo, na Evod mmanda.
Kamati ya
Rufaa za Nidhamu: Prof. Mgongo Fimbo, Ong’wanuhama Kibuta
(m/mwenyekiti), Kanali Mstaafu Idd Kipingu, Dk. Mshindo Msolla, ACP
Jamal Rwambow.
Kamati ya
Nidhamu: Kamanda Mstaafu Alfred Tibaigana (mwenyekiti), Mustafa Kambona
(m/mwenyekiti), Azzan Zungu, Yussu Nzowa na Mohamed Msomali.
Kamati ya
Rufaa za Uchaguzi: Jaji Bernard Luanda (mwenyekiti), Francis Kiwanga
(m/mwenyekiti), A. Steven Semu, Yohane Masalla na Allen Kasamala.
Kamati ya
Uchaguzi: Hamidu Mbwezeleni (mwenyekiti), Moses Kaluwa (m/mwenyekiti),
Mustafa Siani, Hassan Dyamwale na Kitwana Manara.
Kamati ya
Waamuzi: Kapteni Mstaafu Stanley Lugenge (mwenyekiti), Omar Kasinde
(m/mwenyekiti), Said Nassoro, Charles Ndagala na Mohamed Nyama.
Kamanda Mstaafu Jamal Rwambow anaingia kwenye Kamat
0 maoni:
Post a Comment