Mwakilishi wa Shirika la Chakula na Kilimo nchini (FAO) Diana Templeman (katikati) akipata maelezo ya kazi mbalimbali za Shirika hilo kutoka kwa Afisa Habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Usia Nkhoma Ledama wakati alipotembelea banda la Umoja wa Mataifa kwenye maonyesho ya 37 kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Mkufunzu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam ( DIT) Marwa Wambura (katikati) akimuonyesha Mwakilishi wa Shirika la Chakula na Kilimo nchini (FAO) Diana Templeman (kulia) malighafi za ngozi zinazotumika kutengeneza bidhaa mbalimbali na wanafunzi wa Chuo hicho ambapo mafunzo hayo yanadhaminiwa na kuratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuendeleza viwanda Duniani (UNIDO).
Mwakilishi wa Shirika la Chakula na Kilimo nchini (FAO) Diana Templeman akiangalia viatu vya ngozi vilivyotengenezwa na wanafunzi wa Chuo cha DIT kwenye banda la Umoja wa Mataifa kwenye maonesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya bidhaa za ngozi zinazotengenezwa na Wanafunzi wa Chuo cha DIT cha Mwanza.
Mwakilishi wa Shirika la Chakula na Kilimo nchini (FAO) Diana Templeman akizungumza na waandishi habari ambapo amefafanua changamoto mbalimbali zinazoikabili dunia katika mabadiliko ya tabianchi ambapo wao kama Umoja wa Mataifa wanafanya kazi ya kuelemisha Umma, Wakulima, Wafanyabiashara na Wasindikaji jinsi ya kuelelewa mabadiliko ya tabianchi katika kukabiliana na tatizo la uhaba wa njaa duniani na upatikanaji wa chakula. Kulia ni Mratibu wa kazi za vijana vijijini katika masuala ya Kilimo, Uvuvi na Ufugaji wa FAO Bw.Eliamoni Lyatuu.
Afisa habari wa Kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini (UNIC) Usia Nkhoma Ledama akitoa ufafanuzi wa vipeperushi mbalimbali vinavyozungumzia kazi zinazofanywa na shirika hilo hapa nchini kwa baadhi ya vijana na watoto waliotembelea banda hilo leo kwenye maonesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar.
Baadhi ya watoto waliotembelea banda la Umoja wa Mataifa wakifurahia picha.
0 maoni:
Post a Comment