Mshindi wa Redds Miss Temeke 2013, Sviona Nyameyo (katikati), ambaye ni
mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(UDSM), akiwa na mshindi wa pili, Narietha Boniface, mwanafunzi wa
Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba Muhimbili (MUHAS), na mshindi wa tatu,
Latifa Mohamed ambaye ni muhitimu wa kidato cha sita baada ya kutangazwa
washindi katika shindano hilo lililofanyika viwanja vya Sigara
Chang'ombe Dar es Salaam juzi
MREMBO Sylona
Nyameyo juzi usiku alifanikiwa kutwaa taji la Redd’s Miss Temeke lililofanyika
katika Ukumbi wa TCC Changombe, jijini Dar es Salaam.
Sylona aliye
mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM),
akisomea mambo ya sheria alifanikiwa kuwashinda warembo wengine na kufanikiwa
kujitwalia taji hilo.
Katika shindano
hilo lililokuwa na upinzani mkali, ulioambatana na burudani za kumwaga,
ilishuhudiwa nafasi ya pili ikienda kwa Marietha Boniface, ambaye naye ni
mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUCHS).
Nafasi ya tatu
ilikwenda kwa Latifa Mohammed ambaye amemaliza kidato cha sita mwaka huu, hivyo
warembo hao kujihakikishia nafasi ya kuingia katika fainali za Redd’s Miss
Tanzania.
Ushindani
ulionekana dhahiri katika shindano hilo, ambapo warembo walikuwa wakichuana
mno, huku mashabiki waliojitokeza hapo wakijikuta wakishangilia muda wote.
Akizungumza
mara baada ya kuvikwa taji hilo, Sylona alisema amefurahishwa mno na matokeo
hayo na atahakikisha hawaangushi wakazi wa Temeke katika shindano la Redd’s
Miss Tanzania.
“Nilijua toka
mwanzo lazima niwashinde, maana nilijiamini na niliona nina vigezo vyote, sasa
ni wakati wa kwenda kupambana katika Redd’s Miss Tanzania ili kurudisha heshima
ya Temeke,” alisema.
Shindano la
Redd’s Miss Tanzania kwa sasa linadhaminiwa na kinywaji cha Redd’s Original
kinachozalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
0 maoni:
Post a Comment