Wachezaji 6 nyota ( waliokaa) waliochaguliwa kuhuduria Clinic
itakayoongozwa na makocha wa kabla ya Manchester united wakiwa katika
picha ya pamoja mara baada ya kutangazwa katika final za Airtel Rising
stars zilizofanyika katika katika viwanja vya karume jijini Dar es
saalam.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amos Makala
akikabidhi kombe la ubingwa wa Airtel Rising Stars kwa nahaodha wa timu
ya Mwanza Kelvin Faru kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar
mwishoni mwa wiki.
Timu ya Mwanza ikifurahia ushindi mara baada ya kuibuka mabingwa wa fainali za Airtel Rising Stars kwa mwaka 2013
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colaso akiongea wakati wa
kufunga michuano ya Fainali ya mashindano ya Airtel Rising Stars katika
viwanja vya karume jijini Dar es saalam
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amos Makala
akiongea wakati wa kufunga michuano ya Fainali ya mashindano ya Airtel
Rising Stars katika viwanja vya karume jijini Dar es saalam
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amos, akifatiwa na Raisi wa TFF sir Leodgar Tenga pamoja na Mkurugenzi
Mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colaso wakikangua timu kabla ya kucheza
mechi ya finali katika michuano ya Airtel Rising Stars , mechi ilikuwa
kati ya Morogoro na Mwanza
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amos akiongea na wachezaji kabla ya kuanza mechi za fainali
Mlinzi wa Mwanza Ally Mnasi (kushoto) akipambana na Evance Robert wa Morogoro wakati wa fainali kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar mwishoni mwa wiki. Mwanza walishinda 1-0.
Mchezaji Kelvin Matale wa Mwanza (kushoto) akichuana na Dickson Mwesa wa of Morogoro wakati wa fainali kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar mwishoni mwa wiki. Mwanza walishinda 1-0.
Rais wa TFF Leodegar Tenga akimvisha medali kocha wa timu ya taifa
ya vijana Jacob Michaelsin kutambua mchango wake kwenye mashndano ya
Airtel Rising Stars ngazi ya Taifa yaliyomalizika uwanja wa Karume
mwishoni mwa wiki
Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Tanzania Levi Nyakundi akikabidhi
mfano wa hundi kwa mchezaji bora wa Airtel Rising Stars Anna Hebron
kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Timu
ya Mwanza wavulana imeibuka kidedea katika michuano ya Taifa ya vijana
chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars baada ya kuifunga
Morogoro 1-0 katika mechi ya fainali iliyofanyika kwenye uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Nayo timu
ya Kinondoni wametwaa taji la wasichana kwa kuifunga Ilala 1-0.
Goli
pekee la Mwanza lilifungwa na mshambuliaji machachari Athanas Mdam kwa
shuti kali katika dakika ya 34. Mdam amejizolea sifa kem kem baada ya
kuonyesha uwezo mkubwa wa kufunga magoli na kutangazwa kuwa mfungani
bora wa fainali hizo.
Mbali
na Mdam, wachezaji wengine waliong’aa katika mashindano hayo na
kuchaguliwa na jopo la makocha ni Arafat Mussa (mlinda mlango bora)
kutoka Kinondoni na Omary Hussein (mchezaji bora) kutoka Ilala.
Vile
vile wachezaji sita (wasichana watatu na wavulana watatu) wamechaguliwa
kuiwakilisha Tanzania kwenye kliniki ya kimataifa ya soka kwa vijana
itakayofanyika Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo na kusimamiwa na makocha
kutoka shule za mafunzo ya soka za Manchester United. Wachezaji hao ni
Anna Hebron, Niwael Halfan, Shelda Boniface, Athanas Mdam, Thomas
Chindeka na Omary Hassan.
Wakati
huo huo Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limetaja majina ya
timu za wavulana na wasichana yakayofanyiwa mchujo ili kupata wachezaji
16 kutoka kila upande kwa ajili ya kwenda kushiriki michuano ya
kimataifa ya Airtel Rising Stars nchini Nigeria mwezi Septamba.
Wachezaji
hao kwa upende wa wavulana ni Arafat Mussa, Fred Bakari, Emmanuel
Innocent na Willy Karolo (Kinondoni), Aziz Hassan, Omary Hussein, Joseph
Mushi, Saddy Said na Said Danda (Ilala), Rothan Mkanwa, Petro Mgaya,
George Chota, Ramadhani Kondo na Optamus Lupekenya (Morogoro), Bruno
Shayo, Luseke Kiggi, Martini Lusseke na Athanas Mdam (Mwanza), Thomas
Chindeka, Miraji Kingaye na Salum Issa (Temeke) na Michael Bosco
(Mbeya).
Wasichana
ni Najihati Abbas, Stumai Abdallah, Anastazia Anthon, Tatu Iddi, Shelda
Boniphace, Rehema Yahya na Anna Bebron (Kinondoni), Niwael Halfan,
Amina Ramadhan, Latifa Ahmed na Alafa Abdul (Temeke), Vumilia Maharifa,
Donisia Daniel, Maimuna Khamis na Amina Ally Ilala), Khadija Hiza
(Tanga), Mwamvita Tabago, Shakila Hashimu na Zainabu Bakari (Kigoma),
Shamimu Ally na Farida Mohamed (Ruvuma).
Akiongea
wakati wa ufungaji wa mashindano hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel
Tanzania Sunil Colaso alisema kuwa kliniki na mashindano ya Nigeria
yatawapa fursa zaidi ya kujifunza na kupata uzoefu na kusisitiza nia ya
kampuni ya Airtel kuendeleza kudhamini mashindano hayo.
Naye
mgeni rasmi Naibu Waziri wa Habari, Viajana, Utamaduni na Michezo Amos
Makala aliwataka vijana kuonyesha vipaji vyao na kuyataka makapuni
mengine kujitokeza kudhamini michezo. Wito wake uliungwa mkono wa Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) Leodegar Tenga.
0 maoni:
Post a Comment