Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga atakuwa
mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa kozi ya mpira wa miguu wa ufukweni (beach
soccer) itakayoanza kesho (Julai 9 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
Kozi
hiyo itafanyika kwa wiki nzima kwenye klabu ya Escape iliyoko karibu na
Safari Carnival, Mikocheni karibu na makao makuu ya Jeshi la Kujenga
Taifa (JKT)- JKT Mlalakuwa. Uzinduzi utafanyika saa 3 kamili asubuhi.
Washiriki
wa kozi hiyo itakayokuwa chini ya wakufunzi kutoka Shirikisho la
Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ni 60 ambapo 30 ni makocha wa mpira
wa miguu na 30 wengine ni waamuzi wa mpira wa miguu.
Wakufunzi
hao wa FIFA ni Angelo Schirinzi kutoka Uswisi kwa upande wa makocha
wakati George Postmar kutoka Uholanzi ndiye atakayewanoa waamuzi.
PROGRAMU YA MAZOEZI YA TAIFA STARS.
Taifa
Stars chini ya Kocha Kim Poulsen inaendelea kujinoa jijini Dar es
Salaam tayari kuikabili Uganda (The Cranes) katika mechi ya kufuzu kwa
Fainali za Afrika kwa Wazhezaji wa Ligi za Nyumbani (CHAN) itakayochezwa
Jumamosi (Julai 13 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ratiba ya mazoezi kwa Taifa Stars ni kama ifuatavyo;
Jumanne- Julai 9 mwaka huu Saa 9 alasiri Uwanja wa Taifa
Jumatano- Julai 10 mwaka huu Saa 9 alasiri Uwanja wa Taifa
Alhamisi- Julai 11 mwaka huu Mapumziko
Ijumaa- Julai 12 mwaka huu Saa 10 jioni Uwanja wa Taifa
0 maoni:
Post a Comment