Monday, July 22, 2013

REHAB INAYOWANUSURU VIJANA NA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA, YAPUNGUZA MATEJA TANGA

Idadi kubwa ya vijana wanaojiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya inaweza kupungua ama kuisha kabisa endapo waathirika wa utumiaji wa dawa hizo watatumika kutoa elimu kwa vijana wenzao ambao bado hawajaingia katika janga hilo ambalo ni hatari sana kwa nguvu kazi ya taifa.
Vijana wa walioacha kutumia dawa za kulevya wakiomba dua kabla ya kuzungumza na mwandishi wa habari hizi Dotto Kahindi wa kwanza kulia
 
Tone Media kupitia TANGA YETU imefika katika kituo cha watumiaji wa dawa za kulevya (Rehab, SOBER HOUSE) jijini Tanga ambao wanatoa mbinu na elimu ya kutorudia kutumia dawa hizo ambazo zinaathiri na kugharimu maisha ya vijana wengi.
 Mwenyekiti wa SOBER HOUSE, Ibrahim Daga akifafanua jambo kwa mwandishi wa habari (hayupo pichani)

Vijana wadogo ambao pengine sasa wangekuwa wakilitumikia taifa katika mambo mbalimbali walijikuta katika janga hili la dawa za kulevya kutokana na sababu mbalimbali wengine wakirubuniwa na marafiki, tamaa, kwenda na wakati, unywaji pombe na uvutaji bangi ambao uliwapeleka moja kwa moja katika matumizi ya dawa hizo.
Ibrahimu Daga ambaye ni Mwenyekiti wa Rehab SOBER HOUSE jijini Tanga anasema kituo hicho hulea watu 35 na kuwapatia elimu ya namna ya kuishi bila kurudia matumiazi ya dawa hizo, mafunzo ambayo hudumu kwa miezi minne.
Anasema kuwa kituo hicho hakijapata msaada wowote kutoka serikalini hasa mamlaka zinazohusika na dawa za kulevya na kwamba kinajiendesha kwa michango ya wazazi wa waathirika.
“Tunahitaji sana kuungwa mkono na serikali hasa katika upande wa kupata chakula kwa hawa vijana tulionao, lakini katika mipango ya muda mrefu tunahitaji eneo kubwa kwajili ya kujenga Rehab itakayochukua watu wengi zaidi” anaeleza Ibrahim
Meneja wa Rehab hiyo Salum Amour anasema mahitaji makubwa katika rehab hiyo ni kupata elimu ya ujasiliamali, biashara, kilimo na ufugaji kwa waathirika hao ili baada ya kumaliza muda wa Rehab wawe na uwezo wa kuendesha maisha yao hata baada ya kurejea katika hali zao za kawaida.
Miongoni mwa shughuli wanazojifunza ni usafi na kupika

 Vijana hawa wanatoa ujumbe mzito kwa vijana wenzao, wakisema USIJARIBU KUFIKIRIA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA NI HATARI.
Meneja wa Rehab hiyo Salum Amour (mwenye t-sheirt nyekundu) akizungumza na mwandishi wa habari
Nyumba inayotumika kuhifadhia vijana hao
Viongozi wa serikali kuanzia ngazi ya Wilaya, Mkoa na Kitaifa ni jukumu lenu sasa kuhakikisha kuwa mnaunga mkono jitihada za Rehab hii kwa kusaidia kuboresha hudumu ikiwemo chakula ili malengo ya kumaliza tatizo la mateja mitaani yafanikiwe, PESA ZA DAWA ZA KULEVYA NA UKWIMWI ZINAKWENDA WAPI??? Walengwa ndio hawa hamuwaoni?
Picha Zote na Tanga Yetu

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU