Naibu Waziri wa
Fedha, Bi. Saada Mkuya Salum (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC,
Bi. Mizinga Melu (kushoto kwake) wakichukua mlo wa futari pamoja na baadhi ya
wateja wa benki hiyo katika hafla ya futari iliyoandaliwa na NBC kwa wateja
wake jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Naibu Waziri wa Fedha, Bi. Saada Mkuya Salum (kushoto) akizungumza
na Mjumbe wa Bodi ya Benki ya NBC, Dk Kassim Hussein (kulia) wakati wa hafla ya
futari iliyoandaliwa na NBC kwa wateja wake jijini Dar es Salaam. Wa pili
kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Bi. Mizinga Melu na Mkuu wa
Masoko na Mawasiliano, Bi. Mwinda Kiula Mfugale.
Mkuu wa Huduma za
Kibenki kwa kufuata kanuni za Kiislamu wa Benki ya NBC, Yassir Masoud (wa pili
kushoto) pamoja na baadhi ya wateja wa benki hiyo, wakichukua mlo wa futari
katika hafla ya futari iliyoandaliwa na NBC kwa wateja wake jijini Dar es
Salaam mwishoni mwa wiki.
Naibu Waziri wa Fedha, Bi. Saada Mkuya Salum (kulia),
akimsilikiliza Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya nbc, Mwinda Kiula Mfugale
(kushoto) katika hafla ya futari iliyoandaliwa na NBC kwa wateja wake jijini humo
mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Huduma za Kibenki kwa kufuata kanuni za Kiislamu
wa Benki ya NBC, Yassir Masoud (katikati) akiteta jambo na Meneja Uhusiano wa
benki hiyo, Eddie Mhina wakati wa hafla ya futari waliyoiandaa kwa wateja wao jijini
Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mjumbe wa Bodi ya NBC, Dk. Kassim Hussein.
Baadhi ya wateja wa benki ya NBC, wakila futari waliyoandaliwa
na benki hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
0 maoni:
Post a Comment