Shirikisho la soka nchini TFF limesema haliko tayari kumpokea mcheza Kazimoto katika kikosi cha timu ya Taifa baada ya mchezaji huyo kutoroka kambini mara baada ya mchezo wa TANZANIA na UGANDA kumalizika na Tanzania kuchapwa bao moja kwa bila mchezo uliofanyika uwanja wa Taifa Jijini DSM.
Katibu mkuu wa TFF Angetile Osiah amesema mchezaji huyo imeitia aibu kambi ya Stars kwa kutoroka hivyo Tff haitakuwa tayari kuendelea naye katika kikosi cha timu ya Taifa.
Amesema mchezaji huyo alitakiwa kuanga kwani hata akipata timu hata weza kucheza mpaka apate kibari kutoka Tff na klabu yake ya Simba.
0 maoni:
Post a Comment