Wednesday, August 28, 2013

GRAND MALT YAMWAGA VIFAA LIGI KUU ZANZIBAR

 Mwakilishi wa timu ya KMKM ya unguja  Said Mfaume akipokea jezi toka kwa Waziri wa habari,utalii na michezo Zanzibar Said Mbarouk tayari kabisa kwa kuanza kwa ligi kuu ya Grandmalt Zanzibar,Kulia ni meneja masoko wa GrandMalt Fimbo buttala na Rais wa ZFA Ravia Faina
 Mwakilishi wa timu ya Mafunzo  ya pemba  Khamis Ally akipokea jezi toka kwa Waziri wa habari,utalii na michezo Zanzibar Said Mbarouk tayari kabisa kwa kuanza kwa ligi kuu ya Grandmalt Zanzibar,Kulia ni meneja masoko wa GrandMalt Fimbo buttala na Rais wa ZFA Ravia Faina
 Mwakilishi wa timu ya jamhuri  ya pemba  Abdallah Abeid  akipokea jezi toka kwa Waziri wa habari,utalii na michezo Zanzibar Said Mbarouk tayari kabisa kwa kuanza kwa ligi kuu ya Grandmalt Zanzibar,Kulia ni meneja masoko wa GrandMalt Fimbo buttala na Rais wa ZFA Ravia Faina.
KINYWAJI kisicho na kilevi cha Grand Malt, walio wadhamini wa Ligi Kuu ya Zanzibar maarufu kama ‘Grand Malt Premier League’ jana walikabidhi rasmi vifaa kwa timu 12 zinazoshiriki ligi hiyo katika hafla iliyofanyika hoteli ya Bwawani, mjini hapa.
 
Mbali na kumwaga vifaa hivyo, Grand Malt pia wameamua kufanya kweli zaidi kwa kuongeza udhamini wao kwa waamuzi na uendeshaji wa ligi, ambapo msimu huu watatoa kiasi cha Sh milioni 200 kutoka Sh milioni 140 za msimu uliopita.
 
Hafla hiyo maalumu ya kukabidhi vifaa na kutangaza kiasi hicho kipya cha uendeshaji wa ligi,  ilihudhuriwa na viongozi na wanamichezo mbalimbali wakiongozwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Saidi Ali Mbarouk.
 
Akizungumza katika hafla hiyo, Mbarouk alisema wamefurahishwa mno na Grand Malt kwa kuongeza udhamini wao pamoja na kutoa vifaa bora vya michezo kwa timu zote zishiriki.
 
“Tuna uhakika sasa soka ndani ya Zanzibar itazidi kusonga mbele, ombi lenu kwenu ZFA (Chama cha Soka Zanzibar), pamoja na wadau wote kutumia fursa hii kuhakikisha tunafika kule tunakokutaka.
 
“Nawasifu zaidi Grand Malt kwa kuendelea kudhamini Ligi Kuu ya Zanzibar nah ii inadhihirisha tuko nao pamoja kwa mambo mengi, nasi pia tunapaswa kuwaunga mkono kwa kutumia kinywaji chao,” alisema.
 
Mkurugenzi wa Masoko wa Grand Malt, Kushillah Thomas naye alisema, kinywaji hicho kitaendelea kushirikiana na watu wa Zanzibar katika kuhakikisha wanafanikiwa kwenye malengo yao.
 
“Udhamini huu ni mwanzo tu na tunaamini utasaidia kwa kiwango kikubwa kufanikisha malengo ya soka ya Zanzibar,” alisema.
 
Viongozi wa ZFA nao walikiri kufurahishwa na udhamini huo na kusema, wanaamini Ligi Kuu ya Grand Malt msimu huu itakuwa na ushindani mkubwa zaidi.
 
KMKM ndio waliofanikiwa kutwaa ubingwa huo msimu uliopita, wakiwa ni mabingwa wa kwanza toka kuanza kwa udhamini wa Grand Malt.
 
Mbali na KMKM timu nyingine zinazoshiriki ligi hiyo ni Fuoni, Chuoni, Polisi, Malindi (Bandari), Zimamoto, Mafunzo, Jamhuri, Chipukizi, Kizimbani, Mtende na Miembeni.
 
Kinywaji cha Grand Malt kisicho na kilevi ndio walioingia mkataba wa kudhamini ligi hiyo, hivyo kujulikana kama Ligi Kuu ya Grand Malt.



0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU