Wednesday, August 28, 2013

WALIMU WAWILI NA WAKULIMA WAWILI WAIBUKA WASHINDI WA PROMOSHENI YA AIRTEL YATOSHA


Washindi wa siku wa shilingi milioni moja wa promosheni ya Airtel yatosha bwana Thomasi Joackim Chali na Abdallah Omari Muhomba kwa pamoja wakionyesha furaha mara baada ya kukabithiwa zawadi za pesa
taslimu baada ya kuibuka washindi wa siku wa promosheni ya Airtel yatosha.
Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando akiongea na moja ya washindi wakati Airtel ilipochezesha droo ya saba ya washindi wa shilingi milioni moja kila siku wa promosheni ya Airtel yatosha
ambapo mpaka sasa zaidi ya shilingi million 44 zimeshatolewa. Akishuhudia ni Msimamizi wa bodi ya michezo ya Bahati nasibu.

 *   Zaidi ya shilingi million 39 bado kushindaniwa.
 *   Na washindi wa wiki ya sita wakabidhiwa zawadi zao.

Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel imetangaza  washindi wake saba wa wiki ya saba ya  Airtel Yatosha  promosheni na kukabidhi zawadi za  washindi wa wiki ya sita wa promosheni ya  Airtel Yatosha.

Airtel imechezesha droo ya wiki ya saba ya promosheni ya Airtel yatosha Jana  katika ofisi za makao makuu ya Airtel morocco jijini Dar es saalam ambapo wateja saba  wameibuka washindi wa kitita  cha
shilingi million 1 kila mmoja.

Washindi hao ni pamoja na Theresia Martine Komba wa Morogoro -Mkulima, John Kimoro wa kondo Dodoma -Mwalimu, Yohanna Masunga Zengo wa Maswa Shinyanga -Mkulima, Isabellah Joseph wa Chamwino Dodoma  -Mwalimu, Nassor Mohammed Nassor  wa Kariakoo DSM -Mfanyabiashara, Modest Laurian Mussa wa Bukoba Kagera  -Mfanyabiashara na  Masanja Mwanamenda
wa Nkyala Singida -Mfanyabiashara.
Wakati huo huo Airtel imeendelea kuwazawadia wateja wake kupitia promosheni ya Airtel Yatosha ambapo washindi wa wiki ya sita nao walikabidhiwa zawadi zao ambapo kila mmoja aliondoka na shillingi
milioni moja.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo katika ofisi za makao makuu ya  Airtel  bwana Abdallah Omari Muhomba  mmoja wa washindi  wa million  1 alisema, "nashindwa jinsi ya kuongea lakini nawashukuru sana Airtel kwa kuweza kunizawadia shilingi milioni 1 ambazo kwangu  nikama ndoto.
 Nategemea kutumia pesa hizi kujiendeleza kiuchumi na maaendeleo ya familia yangu. Binafsi nachukua fursa hii kuwaasa watanzania kushiriki katika promosheni hizi za Airtel na kwa hakika wataamka washindi kama
mimi hivi leo".

Kwa upande wake bwana Thomas Joachim Chali ambaye pia ni Mshindi wa wiki ya sita alisema, "anawashukuru Airtel kwa kuanzisha promosheni yaAirtel Yatosha , na kuahidi kuzitumia pesa zake kuendeleza na kupanua biashara kwa kuwa hiyo ndio shughuli kubwa anayoifanya"

Akiongea wakati wa makabidhiano hayo kwa washindi hao Meneja uhusiano wa Airtel bwana Jackson Mmbando alisema, "leo tunao washindi saba waliojishindia shilingi milioni 1 kila moja katika droo ya wiki.
Tumeendelea kushuhudia watanzania na wateja wetu wakiibuka mamilionea kila siku na kila mwezi kupitia promosheni hii ya Airtel Yatosha.

Tunaahidi kuendelea kuwazawadia wateja wetu huku tukiboresha huduma zetu , na kuwapata wateja wetu huduma bora zenye gharama nafuu kupitia huduma yetu poa ya Airtel Yatosha inayomuwezesha mteja kuwasiliana na mitandao mengine ya simu za mkononi kwa bei poa na kupata vifurushi
vya maongezi bila kulipia gharama ya ziada". Aliongeza Mmbando.

Promosheni ya Airtel Yatosha bado inaendelea na wateja wetu wa Airtel Yatosha bado wananafasi ya kuendelea kujishindia pesa taslim na Nyumba  mbili za kifahari zilizopo Kigamboni  bado kushindaniwa.

Droo itakayomchagua mshindi wa nyumba kwa mwezi huu inatarajiwa kuchezeshwa tarehe 5/9/2013 saa tano asubuhi. hii itachagua mshindi mmoja kati ya wateja wote waliotumia huduma ya Airtel yatosha kwa
mwezi huu.

Ili mteja wa Airtel aweze kushiriki  anatakiwa kujiunga na vifurushi vya Airtel Yatosha kwa kupiga *149*99# na kujiunga na vivurushi vya Airtel Yatosha. Kila unapojiunga na kifurushi unaingia moja kwa moja
kwenye droo ya kushinda.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU