Mchakato
wa uchaguzi wa kamati mpya ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) unatarajiwa kutangazwa kesho (Agosti 13 mwaka huu).
Mwenyekiti
wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Hamidu Mbwezeleni atakutana na Waaandishi
wa Habari kwenye ofisi za TFF saa 6 kamili mchana ambapo mbali ya
mchakato utakavyokuwa anatarajia kutangaza tarehe mpya ya uchaguzi huo
ambao awali ulitarajiwa kufanyika Septemba 29 mwaka huu.
Kamati
ya Uchaguzi ya TFF ilikutana Jumapili (Agosti 11 mwaka huu) na
inatarajia kuwa na kikao kingine leo (Agosti 12 mwaka huu) ambapo pamoja
na mambo mengine itazungumzia maandalizi ya uchaguzi huo.
Mbali
ya Mbwezeleni, wajumbe wengine wa Kamati hiyo ni Moses Karuwa (Makamu
Mwenyekiti), Mohamed Sinani, Chabanga Dyamwale na Kitwana Manara.
MAGORI, LINA WAINGIA KAMATI ZA CAF
Watanzania
Crescentius Magori na Lina Kessy wameteuliwa kuwa wajumbe kwenye kamati
ndogondogo (standing committees) mpya za Shirikisho la Mpira wa Miguu
Afrika (CAF) zilizotangazwa juzi na Katibu Mkuu wa shirikisho hilo
Hicham El Amrani.
Magori
na Lina ambao ni wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF watakuwa kwenye
kamati hizo kwa kipindi cha miaka miwili (2013-2015). Magori ameteuliwa
kuwa mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Mashindano ya Mpira wa Miguu wa
Ufukweni (Beach Soccer) wakati Lina ameingia kwenye Kamati ya Maandalizi
ya Mpira wa Miguu kwa Wanawake.
Makamu
wa Rais wa TFF, Athuman Nyamlani ameteuliwa tena kuwemo kwenye Bodi ya
Rufani ya CAF yenye wajumbe 12 kwa kipindi kingine cha miaka miwili.
Nyamlani alikuwepo kwenye bodi iliyopita, na itaendelea kuwa chini ya
uenyekiti wa Prosper Abega kutoka Cameroon.
Rais
wa TFF, Leodegar Tenga ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya
CAF yuko kwenye kamati tano za Shirikisho hilo. Kamati hizo ni Kamati ya
Fedha ambayo ni Makamu Mwenyekiti na Kamati ya Maandalizi ya Fainali za
Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN).
Kamati
nyingine ni Kamati ya Masoko na Televisheni ambayo ni Mwenyekiti,
Kamati ya Ufundi na Maendeleo, na Kamati ya Ushauri na Vyama Wanachama
wa CAF.
KAMATI YA SHERIA KUPITIA USAJILI
Kamati
ya Sheria na Hadhi za Wachezaji chini ya Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa
inakutana leo jioni (Agosti 13 mwaka huu) na kesho (Agosti 14 mwaka
huu) kupitia na kufanyia uamuzi usajili wa wachezaji wenye matatizo.
Hatua
ya kwanza ya usajili imeshamalizika wakati hatua ya pili ya usajili
inaanza kesho (Agosti 14 mwaka huu) ikihusisha wachezaji ambao watakuwa
hawajasajiliwa katika Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu na wale kutoka nje
ya Tanzania.
Hivyo,
dirisha la uhamisho kwa wachezaji wa kimataifa litafungwa baada ya
hatua ya pili ya usajili kumalizika Agosti 29 mwaka huu.
0 maoni:
Post a Comment