Mkuu wa
Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana(kulia) akimkabidhi cheti, Mtendaji wa
Kata ya Makumbusho Wilaya ya Kinondoni , Husna Nando wakati wa hafla ya
kukabidhi vyeti kwa wahitimu wa mafunzo ya ulinzi shirikishi Dar es Salaam jana.Picha na Michael Machellah
Mhitimu wa
mafunzo ya Ulinzi shirikishi kata ya Makumbusho Wilaya ya Kinondoni ,Ally
Vumbi(kushoto)akipiga saluti kwa Mkuu wa Wilaya, Jordan Rugimbana mara baada ya
kutunukiwa cheti baada ya kumaliza mafunzo ya ulinzi shirikishi Dar es Salaam
jana.
Mkuu wa
Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana (kushoto) akimkabidhi cheti cha shukrani
Mkuu wa mafunzo ya Ulinzi Shirikishi Kata ya Makumbusho Wilaya ya Kinondoni,
Koplo Ibrahim Omari wakati wa hafla ya kukabidhi vyeti kwa wahitimu wa mafunzo
ya ulinzi shirikishi Dar es Salaam jana.
Mkuu wa
mafunzo ya Ulinzi Shirikishi Kata ya Makumbusho Wilaya ya Kinondoni, Koplo
Ibrahim Omari akitoa shukrani kwa Mkuu wa Wilaya Jordan Rugimbana kwa kupisha
zoezi la kutoa mafunzo ya ulinzi shirikishi kuwa la Wilaya nzima wakati wa
hafla ya kukabidhi vyeti kwa wahitimu wa mafunzo ya ulinzi shirikishi Dar es
Salam jana.
Baadhi ya
Polisi jamii wa Barabara ya Kilwa,wakiwa kwenye gwaride na mbwa waliopewa
mafunzo maalumu ya ulinzi shirikishi wakati wa hafla ya kukabidhi vyeti kwa
wahitimu wa mafunzo ya ulinzi shirikishi wa Kata ya Makumbusho Mwananyamala
Kinondoni jijini Dar es Salaam jana.
Mkuu wa
Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana(kushoto) akizungumza na wahitimu wa
mafunzo ya Ulinzi shirikishi na wakati wa Kata ya Maakumbusho wakati wa hafla
ya kukabidhi vyeti kwa wahitimu hao Mwananyamala jijini Dar es Salaam jana.
MKUU wa
Wilaya ya Kinondoni,Jordan Rugimbana ametoa muda wa miezi mitatu,Kata zote za
Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam ziwe zimeshaanzisha vikundi vya Ulinzi
shirikishi na kiongozi yeyote atakaekaidi agizo hilo basi anashiriana na
wahalifu.
Rugimbana
aliyasema haya wakati wa hafla ya kukabidhi Vyeti kwa wahitimu wa 40 waliofuzu
mafunzo ya ulinzi shirikishi kata ya Makumbusho Wilaya ya Kinondoni jijini Dar
es Salaam ambapo pia ametoa fursa ya baadhi ya wahitimu kwenda Polisi Kilwa
Road kupata elimu ya kutumia Mbwa katikka kazi ya ulinzi shirikishi baada ya
kuvutiwa na vijana wa Polisi jamii walioonyesha gwaride pamoja na mbwa katika
hafla hiyo.
Alisema
Rugimbana,”Nendeni mkafanye kazi na mtakapo pata kikwazo niambieni niko tayari
kudili na mtu wa yeyote,kafanyeni kazi kwa ufasaha muipe sifa Kata ya
Makumbusho na Wilaya nzima ya Kinondoni kwa kumaliza kabisha swala la
uhalifu,madawa ya kulevya pamoja na
usafi wa mazingira”.
Rugimbana
alisema kuanzia sasa mtu yeyete atakayekamatwa kwa uchafuzi wa mazingira faini
ni fedha taslimu shilingi 50,000/= na hiyo pesa ni ya kwako wewe uliyemkamata.
Aidha Mkuu
wa Wilaya alichangia mfuko wa Polisi jamii Kata ya Makumbusho kiasi cha Shilingi
1,000,000/= pamoja na kuwa mlezi wa Polisi jamii wa Wilaya nzima.
Akitoa
shukrani kwa Mkuu wa Wilaya,Diwani wa Kata ya Makumbusho, Ally Haroub aliwaomba
wakazi wa makumbusho kutoa ushirikiano katika swala la ulinzi shirikishi ili
kupunguza uhalifu, madawa ya kulevya na swala la mazingira kwa kutoa tofauti
zao za kidini,kabila wala umri kwani kipindupindu hakichagui dini ,kabila wa la
Kiongozi.
Mafunzo ya
wahitimu ya vijana wa ulinzi shirikishi yametumia muda wa miezi miwili chini ya
Koplo Ibrahim Omary kutoka kituo cha Polisi Ostarbay yenye madhumuni ya
kuunganisha polisi na jamii ili kufanya kazi kwa umoja na ushirikiano katika
kuondoa kero za uhalifu,kutatua matatizo ya uhalifu na kuondoa hofu ya usalama
wa jamii husika.
Wakisoma
risala wahitimu hao kuwa mafunzo waliyopata ni huduma bora kwa
wateja,ukakamavu,dhana ya polisi jamii,nidhamu,ukamataji salama wa
mhalifu,uwasilishaji taarifa,sheria ndogo nogo za ulinzi,usafi na mazingira na
pia walipata nafasi ya kutembelea kikosi cha mbwa na farasi.
Mwisho walizindua
mfuko wa Ulinzi shirikishi ambao kila mwananchi atakayeguswa na huduma yao
achangie ambayo ni 03201000035 Dar es Salaam Commuty Bank Tawi la Magomeni.
0 maoni:
Post a Comment