Friday, August 30, 2013

NBC BENKI YAZINDUA KITENGO CHA HUDUMA BINAFSI ZA KIBENKI

 Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Kitengo cha Huduma Binafsi za Kibenki kwa Wateja Wakubwa cha benki hiyo jijini Dar es Salaam leo. Kushoto kwake ni  Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Mizinga Melu na kulia kwa Mengi ni Mkuu wa Kitengo hicho, Andrew Massawe.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Mizinga Melu akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Kitengo cha Huduma Binafsi za Kibenki kwa Wateja Wakubwa cha NBC jijini Dar es Salaam
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Mizinga Melu (kushoto) akiwatambulisha baadhi ya maofisa katika kitengo hicho katika hafla hiyo
 Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi (katikati) akifurahi na Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Mizinga Melu (kushoto) na Mkuu wa Idara ya Huduma za Kibenki kwa Wateja Wakubwa na Uwekezaji, Andre Potgieter katika hafla ya uzinduzi wa Kitengo cha Huduma Binafsi za Kibenki kwa Wateja Wakubwa cha benki hiyo jijini Dar es Salaam
 Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi (katikati) akishikana mikono na Meneja Uhusiano wa NBC, Makyalen Marealle katika hafla ya uzinduzi wa Kitengo cha Huduma Binafsi za Kibenki kwa Wateja Wakubwa cha benki hiyo jijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo hicho, Andrew Massawe na Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Mizinga Melu
 Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi (katikati) akihojiwa na waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari mara baada ya uzinduzi wa kitengo hicho. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Mizinga Melu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Mizinga Melu (kulia) akimsindikiza Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi mara baada ya uzinduzi wa Kitengo cha Huduma Binafsi za Kibenki kwa Wateja Wakubwa cha benki hiyo jijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Huduma Rejareja za Kibenki wa NBC, Mmoloki Legodu na Mkuu wa Kitengo hicho, Andrew Massawe.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU