Thursday, August 22, 2013

WANANCHI KILOMBERO WANUFAIKA NA MRADI WA MAJI YA VISIMA

 Akina mama wa Kilombero wakiandaa mlo kwa ajili ya timu za Help for Underserved Communities (HUC) na Lifetime Wells for Ghana Inc., wakati wa ufungaji pampu katika moja ya visima Wilaya ya Kilombero, Morogoro, uliofanyika hivi karibuni. Zaidi kuhusu mrad
 Mtoto toka Kilombero, akifuatilia ufungaji pampu katika moja ya visima 59 uliofanywa na timu za Help for Underserved Communities (HUC) na Lifetime Wells for Ghana Inc., Wilaya ya Kilombero, Morogoro, hivi karibuni.
 Haya twende! Timu ya Help for Underserved Communities (HUC) ikishirikiana na Lifetime Wells for Ghana Inc., wakichimba moja ya visima 59 Wilaya ya Kilombero, Morogoro, huku wakiangaliwa kwa shauku na watoto hivi karibuni. HUC ni asasi isiyokuwa ya kiserikali yenye makao yake Marekani, inayochimba visima kwa kushirikiana na jamii kusaidia upatikanaji wa maji ya kunywa safi na salama mashuleni, vijijini na jamii kwa ujumla.
 Wakazi wa Kilombero wakiangalia kisima kilichochimbwa na Help for Underserved Communities (HUC) kwa ushirikiano na Lifetime Wells for Ghana Inc., Wilaya ya Kilombero, Morogoro, hivi karibuni. Zaidi kuhusu HUC
 imu ya Help for Underserved Communities (HUC), ikishirikiana na Lifetime Wells for Ghana Inc., wakifunga pampu katika moja ya visima 59 Wilaya ya Kilombero, Morogoro, Tanzania huku wakifuatiliwa kwa shauku na watoto hivi karibuni
 Wakaazi wa Kilombero wakichota maji toka katika moja ya visima 59 vilivyochimbwa na Help for Underserved Communities (HUC)/Lifetime Wells for Ghana Inc., Wilaya ya Kilombero, Morogoro, Tanzania, hivi karibuni.

 Wachimba visima toka Help for Underserved Communities (HUC) na Lifetime Wells for Ghana Inc., kama walivyokutwa na kamera yetu Wilaya ya Kilombero, Morogoro, wakati wa uchimbaji visima vya msaada uliotolewa na taasisi hizo hivi karibuni

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU