Tuesday, September 10, 2013

AIRTEL YAENDELEA KUUNGA MKONO DHAMIRA ZA KAMPENI YA USALAMA BARABARANI

Mwaka huu yadhamini tena uchapishaji wa stika za usalala barabarani pamoja na wiki ya usalama barabarani Kampuni ya mitandao ya simu za mkononi nchini, Airtel imetajwa kuwa moja kati ya makampuni ambayo yamekuwa yakishirikiana na serikali kwa dhati katika harakati za kupambana na tatizo la ajali za barabarani.
Akithibitisha madai hayo, Kamanda mkuu wa kikosi cha usalama barabarani, DCP Mohamed R. Mpinga amesema kuwa Airtel imeweza kutoa mchango katika kupunguza wimbi la ajali za barabarani kwa kiasi kikubwa ikitoa ushirikiano katika juhudi mbalimbali zinazofanywa na kikosi cha usalama barabarani kwa dhumuni la kuepusha ajali za barabarani.

"Airtel ni wadau wakubwa wa kampeni za usalama barabarani,  kwa miaka mitano mfululizo na hata mwaka huu 2013 Airtel inaendelea na udhamini wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani. Airtel pia imedhamini vipindi vya elimu ya usalama barabarani katika TV - kumekucha na Jambo Tanzania (ITV na TBC 1) na Radio one.

Pia Airtel kwa kushirikiana na Rotary club na jeshi la polisi usalama barabarani  imedhamini kampeni yenye ujumbe usemao Kuendesha + Simu =
Kifo inayowaasa waendesha vyombo vya moto kutotumia simu wakati wakiendesha magari, vile vile  mwaka jana Airtel ilidhamini mashindano ya mpira wa miguu kwa wapanda pikipiki (Bodaboda) yaliyokuwa na lengo la kutoa elimu ya usalama barabarani kwa waendesha pikipiki ," alisema
DCP Mpinga.

Nae Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel-Tanzania Bi Beatrice Singano Mallya, akizungumza juu ya suala hilo, amesema "Airtel imeamua kushirikiana na serikali katika kuhakikisha inatokomeza kabisa wimbi la ajali za barabarani. Idadi ya vifo vinavyotokea barabarani ni kubwa mno na ndiyo maana Airtel imeamua  kujikita katika kuokoa maisha ya wateja wake na watanzania kwa ujuma. Tunapenda kuwakumbusha watanzania kuwa swala la kupunguza ajali za barabarani ni wajibu wa kila mwananchi  hivyo tutii sheria bila shuruti"  Airtel itaendelea kushirikiana na jeshi la polisi usalama barabarani katika kuhakikisha lengo letu la kupunguza ajali linafanikiwa, tumeanza kuona mafanikio na kwa kiasi Fulani ajali za barabarani zinapungua kulinganisha na miaka iliyopita," alisema Beatrice.

Tumepatiwa Takwimua kwa na ofisi inayoratibu wiki ya nenda kwa usalama barabarani zinabainisha ajali za barabarani zimeweza kupungua kwa kiasi kikubwa tokea mwaka 2011 ambapo Airtel imekuwa ikishirikiana nao katika programu mbalimbali mjini na vijijini, kabla ya hapo tokea mwaka 1995 ajali zilikuwa zikiongezeka kila mwaka kati ya ajali 2,000 na 4,000. Lakini Mwaka 2010 ukilinganisha na  2011 ajali zilipungua kwa 3% na 2011 na 2012 ajali zilipungua kwa 2%.

 Airtel Tanzania inaendelea na kudhamini wiki hii ambapo kwa mwaka huu imejitolea kuchapisha tena stika za usalama barabarani pamoja na kudhamini tena mashindano ya mpira wa miguu ya waendesha bodaboda yajulikanayo kama MPINGA CUP ambayo dhamira yake ni kuunga mkono
juhudi za baraza linaloshughulikia usalama barabarani maalum kwa kutoa elimu kwa watumia vyombo vya moto na waenda kwa miguu barabara zote ili kuepusha ajali.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU