Friday, September 6, 2013

AIRTEL YATANGAZA MSHINDI WA PILI WA NYUMBA YA PROMOSHENI YA AIRTEL YATOSHA.

Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando akiongea na mshindi wa nyumba ya pili wa promosheni ya Airtel yatosha Jishindie nyumba 3 mara baada ya kuibuka mshindi katika droo iliyochezeshwa katika ofisi za Airtel na kushuhudiwa na waandishi wa habari.  bi Anna Gustav Lyimo (29)  Afisa wa benki kuu na mkazi wa Dar es salaamu  ameibuka kuwa mshindi wa nyumba ya kisasa iliyopo kigamboni jijini Dar es salaam , akishuhudia ni Meneja Msoko wa Airtel Aneth Muga ( kulia)  na mwakilishi wa bodi ya michezo ya kubahatisha Emmanuel Ndaki
Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando akiongea na waandishi wa habari wakati wa kuchezesha droo ya pili ya mshindi wa nyumba wa promosheni ya Airtel yatosha Jishindie nyumba 3 ambapo bi Anna Gustav Lyimo (29)  Afisa wa benki kuu na mkazi wa Dar es salaamu  ameibuka kuwa mshindi wa nyumba ya kisasa iliyopo kigamboni jijini Dar es salaam , akishuhudia ni Meneja Msoko wa Airtel Aneth Muga ( kulia)  na mwakilishi wa bodi ya michezo ya kubahatisha Emmanuel Ndaki.

kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imemtangaza Afisa wa Benki Bi Anna Gustav Lyimo (29)  mkazi wa Dar es Salaam kuwa mshindi wa pili wa nyumba aliyepatikana kupitia promosheni maalumu inayofahamika kwa jina la Airtel yatosha shinda nyumba ambapo mshindi huyu atapata nyumba ya kisasa ya vyumba vitatu , iliyojengwa na shirika la National Housing Corporation iliyoko kibada , kigamboni jijini Dar es Saalam
Bi Anna Gustav Lyimo amejishindia nyumba yenye thamani ya shilingi million 685 na kuwa mshindi wa pili kushinda nyumba baada ya Bw. Silvanus Juma kuibuka mshindi wa kwanza mwenzi uliopita.

Akizungumza baada ya kuchezeshwa kwa droo hiyo, Meneja Uhusiano wa Airtel, Bw. Jackson Mmbando alisema Airtel inayo furaha kuchezesha droo ya pili ya nyumba leo na kumpata Bi Anna Gustav Lyimo Kutoka Dar Es Salaam mshindi wa pili wa nyumba kupitia promosheni ya Airtel yatosha shinda nyumba 3 ambayo mpaka sasa inatoa nyumba 2 kwa watanzania huku washindi wengine 56 wakiondoka na shilingi milioni moja kila mmoja. Tunafurahi kuona promosheni hii ikibadilisha maisha ya wateja wetu na familia zao kwa ujumla.

Aliendelea kwa kusema bado wateja wa Airtel wanaweza kuendelea kushindania nyumba moja iliyobaki kwa kujiunga na vifurushi mbalimbali vya Airtel na mwisho wa siku mtu anaweza kuibuka mshindi wa nyumba au kushinda milioni moja kila siku.

Ili kushinda mteja anahitaji kupiga *149*99# na kuchagua kifurushi cha siku, wiki au mwenzi baada ya hapo mteja atakuwa ameingia moja kwa moja katika promosheni ya Airtel yatosha shinda nyumba 3, itakayomuwezesha kujishindia milioni moja kwa kila siku au nyumba kwa mwisho wa mwenzi.

Airtel inaendeleza dhamira yake ya kutoa huduma bora na bei nafuu na kuwazawadia wateja wake nchi nzima  kwa kutumia huduma ya Airtel yatosha, hii ni dhahiri kabisa kwamba promosheni hii imeleta tija na kusaidia kuinua maendeleo yao nay a jamii inayowazunguka Aliongeza Mmbando.

Akielezea furaha yake mshindi huyo wa nyumba Bi Anna Gustav Lyimo alisema, “Ninamshukuru Mungu kwa Bahati hii na noamba Airtel waendelee kuleta mabadiliko kwa wateja wengine kama walivyofanya kwangu.,  nimekuwa nikijiunga na vifurushi vya Airtel yatosha kama huduma lakini sikuwahi kudhani kama ntaweza kushinda, leo nimeamini kuwa promosheni hizi zinamlenga mtu yeyote na unaweza kuabahatika kushinda zawadi kubwa kama hii”
Airtel yatosha promotion bado inaendelea, nyumba mbili zenye thamani ya shilingi milioni 65 kila moja zimeshazawadia kwa wateja na bado nyumba moja kutolewa mwenzi wa Kumi. Zawadi za pesa taslimu kiasi cha shilingi milioni 34 bado kukabithiwa
Airtel Jana imezindua ofa mpya ya kifurushi cha siku cha Airtel yatosha BABA LAO  kinachomuwezesha mteja kuwasiliana na mtandao wowote nchi kwa shililing 499 mteja anapata  dakika 20 za muda wa maongezi , sms 300 na internet MB 125, hii ni ya kwanza na pekee sokoni kutoka Airtel.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU