Baadhi ya
wachezaji wanaoshiriki fainali za
mashndano ya Safari Pool Taifa ngazi ya mkoa, Mkoa wa Mbeya wakiwa kwenye
maandamabo kuingia ukumbini wakati wa
ufunguzi wa fainali hizo zinazofanyika Airport Pub mkoani humo.
Meneja
matukio wa TBL tawi la Mbeya, Godfrey Mwangugulu(kushoto) akizungumza na
wachezaji wa Pool (hawapo pichani) wakati
wa ufunguzi wa fainali za mashindano ya Safari Pool Taifa ngazi ya mkoa
yanayofanyika Airport Pub mkoani humo.Wengine kushoto kwake ni mratibu wa mashindano
hayo, Peter Zacharia,Afisa michezo wa Mkoa wa Mbeya, George Mbijima na
Mwenyekiti wa chama cha Pool Mkoa wa Mbeya, Samweli Aron.
Afisa
michezo wa Mkoa wa Mbeya, George Mbijima akizungumza na wachezaji wa
Pool(hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa fainali za mashindano ya Safari Pool
Taifa ngazi ya mkoa yanayofanyika Airport Pub mkoani humo.Kulia ni Meneja matukio wa TBL tawi la Mbeya, Godfrey
Mwangugulu,mratibu wa mashindano Peter Zacharia na Mwenyekiti wa chama cha Pool
Mkoa wa Mbeya, Samweli Aron.
Afisa
michezo wa Mkoa wa Mbeya, George Mbijima akicheza wakati wa ufunguzi wa fainali za mashindano ya
Safari Pool Taifa ngazi ya mkoa yanayofanyika Airport Pub mkoani humo.Wengine
wanaoshuhudia kushoto kwake ni mratibu wa mashindano , Peter Zacharia na Meneja matukio wa TBL tawi la Mbeya,
Godfrey Mwangugulu
Afisa
michezo wa Mkoa wa Mbeya, George Mbijima akipigiwa makofi mara baada ya
kufuangua rasmi mashindano. humo.Wengine wanaoshuhudia kushoto kwake.
FAINALI za
mashindano ya mchezo wa Pool Taifa zinazodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania
kupitia bia yake ya Safari Lager zimeanza rasmi jana Mkoani mbeya
zikishilikisha vilabu tisa vya mkoani humo.
Akifungua
fainali hizo Afisa michezo wa Mkoa wa Mbeya, George Mbijima aliwaomba wachezaji
kuwa na watulivu na kuzingatia nidhamu ya mchezo ili mwisho wa fainali
apatikane mshindi atakaebeba bendera ya Mkoa wa mbeya kwenye fainali za kitaifa
na arudi na ushindi.
Mbijima
alisema taswila ya mchezo wa Pool si nzuri sana miongoni mwa watu kwani
unatazamwa kama mchezo wa wahuni na hakuna mtu mwingine wa kubalilisha zaidi ya
wachezaji wenyewe,hivyo kuweni na nidhamu ili hata jamii ifike mahala itambue
kumbe pool ni mchezo kama michezo mingine.
Mbijima pia
aliishukuru TBL, kupitia bia ya Safari Lager kwa kuendelea kudhamini mashindano
hayo kwani kwa kufanya hivyo inawafanya vijana kuepuka vitu vingi ikiwemo
uhalifu,kukaa vijiweni bila kazi lakini sasa wananufaika chochote
kutokana na zawadi wanazopata ukizingaatia michezo ni ajira,michezo
burudabi na michezo ni kufahamiana.
Nae Meneja
matukio wa TBL Mbeya,Godfrey Mwangugulu aliwatakia wachezaji michezo mema na
yenye amani mwisho apatikane bingwa wa haki atakaye wakilisha vyema Mkoa wa
Mbeya
Mwisho
Mwenyekiti alivitaja vilabu
vinavyoshiriki fainali za Safari Pool Mkoa wa Mbeya kuwa ni Tunduma Kontena
Klabu,Royal Zambezi Klabu,Royal Glass Klabu,Shooters klabu,Luanch time klabu,Mbeya
snukers klabu,Kizota klabu,Makonde klabu na Terminal Stand klabu.
Zawadi katika fainali hizo upande wa timu,bingwa
atajnyakulia fedha taslimu shilingi 700,000/=,mshingi wa pili 350,000/=,wa tatu
200,000/= na wanne 100,000/ na timu nane zitakazoingia robo fainali zitapata
kifuta jasho cha fedha taslimu shilingi 50,000/= kila moja.
Upande wa
mchezaji mmoja mmoja(Singles), wanaume bingwa atapata zawadi ya fedha taslimu
shilingi 350,000/=,wa pili 250,000/=,wa tatu 150,000/= na wanne 100,000/= na
upande wa kinadada bingwa atajinyakulia fedha taslimu shilingi 250,000/=,wa
pili 150,000/=,wa tatu 100,000/= na wanne 50,000/=.
0 maoni:
Post a Comment