Saturday, September 21, 2013

BENDELA ASHAURI VYAMA VYA MICHEZO VIWE NA WADHAMINI WA KUDUMU

 Baadhi ya wachezaji wa Pool kutoka mikoa 17 ikiwakilisha na vilabu 17 nchini wakiwa katika maandamano kuelekea katika Ukumbi wa Tanzanite Morogoro wakati wa ufinguzi wa fainali za kitaifa za Safari National Pool Championships
 Mzamini Mkuu wa mashindano ya Safari National Pool Championships,Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo(wa tatu kushoto),Mwakilishi wa TBL Morogoro,Julius Ngaga(wanne kusho),Mwenhyekiti wa chama cha Pool Mkoa wa Iringa, Salum Kisaku (wa pili kushoto) na Mwamuzi wa kike pekee,Vaileth Mrema(kushoto)  na baadhi ya wachezaji wakiwa katika maandamano ya ufunguzi wa fainali za Pool Taifa Mkoani Morogoro.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Joel Bendela(wa poli kushoto),Meneja wa wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo,Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Pool Taifa(TAPA), Fred Mush na Katibu wa chama cha Pool Taifa , Amos Kafwinga wakiwa katika maandamano ya ufunguzi wa fainali za mashindano ya Safari National Pool Championships jana.

MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendela, amewaasa chama cha Pool Taifa(TAPA), kumkumbatia mdhamini mkuu  wa mhezo wa Pool Taifa, “Safari Lager” kupitia Kampuni kubwa nchini Tanzania Breweries(TBL).
Bendela aliyasema hayo wakati wa ufunguzi wa fainali za mashindano hayo yanayoyofanyika kitaifa Mkoani Morogoro ambapo yeye alialikwa kuwa mgeni rasmi.
Alisema Bendela, vipo vyama vya michezo vingi vinashindwa hata kufanya mashindano kwa mwaka lakini Pool ni mwaka wa sita sasa mnafanya,vipo vyama vingi vya michezo vinalia kwanini mpira wa miguu peke yake ndio unapata udhamini lakini Pool ni mwaka wa sita sasa mnae mzamini na bado mnaendelea nae na baada ya hapa anaipeleka timu ya Tifa kwenye mashindano ya Afrika ya mchezo wa Pool.
Mchezo wowote  ili ukue na kutambulika nchini na Duniani unaanza na mchezaji mwenyewe kuupenda na kuufanya kutoka moyoni kwa kujiheshimu kwanza mwenyewe na kuuheshimu mchezo ndipo hata jamii huudhamini(Self displine anda Tactical displine).

Alisema Bendela yeye kama mdao na mzoefu kwenye tasnia ya michezo na mpaka sasa anashikiria sifa kemkem ambazo hazijawahi kutolewa kwenye rekori anauzoefu wa kutosha na maswala ya michezo,siri ya maendeleo katika michezo ni nidhamu pekee na si vinginevyo.

Mtazamo wa mchezo wa Pool katika jamii siku kadhaa hapo nyuma ulionekana kama mchezo wa kihuni lakini leo mmebadilisha taswira hiyo na sasa mko kwenye mikoa 17 ikiwakilisha na vilabu 17 mkiunganisha na mchezo wa Pool mkiwa mkoani Morogoro katika fainali za kitaifa, hongereni sana TAPA.

Mkuu wa Mkoa pia aliipongeza TBL kupita bia ya Safari Lager kwa kuendelea kudhamini mchezo wa Pool na sasa ni mwaka wa sita ambapo aliomba waendelee kudhamini kwani mchezo huu unaunganisha vijana wengi Tanzania kwa hapo walipofikia kwenye mikoa 17,unaepusha mambo mengi maovu ambayo wangekumbana nayo hawa vijana ni zaidi ya vijana 300 wamekutana Mkoa wa Morogoro na kilicho wakutanisha ni mchezo wa Pool.Endeleeni kudhmini mchezo wa Pool kwani kwa sasa michezo ni afya, michezo ni upendo,michezo ni urafiki,michezo ni matangazo na michezo ni afya.
Bendela aliwakaribisha wote Mkoani Morogoro na kuwaomba wawe na amani kwani Morogoro ni shwari kabisa hewa nzuri baridi kiasi.

Nae Meneja wa Bia ya Safarai Lager,Oscar Shelukindo alimshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kujitokeza kufungua fainali hizo na kuahidi lengo la Safari Lager na kuufanya mchezo wa Pool kuwa mchezo namba moja kama ilivyo Safari Lager bia namba moja Afrika hivyo wataenelea kudhamini mashindano ya Pool daima.

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Pool Taifa, Fred Mushi alimsukuru mdhamini Safari Lager kuendelea kuwadhamini na pia kumshukuru Mkuu wa mkoa kwa changamoto alizozieleza za kumlinda mdhamini na kuahidi wanajitahidi kwa kadri ya uwezo wao kuwaweka sawa vijana kuhakikisha mchezo wa Pool unakuwa chezo namba moja nchini na Afrika kama bia ya Safari Lager.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU