The Tanzanian Team before their first match between Ghana. They lost 2-1 at the Onikan Stadium, Lagos.
The Tanzanian Team before their first match between Ghana. They lost 2-1 at the Onikan Stadium, Lagos.
Lagos
, Septemba 2o , 2013... Timu zote za wavulana na wasichana zimeingia
robo fainali katika michuano ya kimataifa ya vijana chini ya umri wa
miaka 17 ya Airtel Rising Stars yanayofanyika Lagos , nchini Nigeria na
mshindi atapata medali , kombe pamoja na dola za marekani 10,000.
Timu
ya wasichana imetinga robo fainali baada ya ya kutoka sare ya 1-1 dhidi
ya Malawi jana na kumaliza na pointi nne katika kundi ambapo timu ya
Uganda ikishika uskani kwa point sita. Wakicheza kwa kujiami timu ya
wasichana ya Tanzania ilipata goli katika dakika ya 17 kupitia kwa
mshambuliaji hatari Shelda Boniface , kabla ya Malawi kuzawazisha dakika
ya saba katika kipindi cha pili.
Mshambuliaji
mwenye uwezo wa hari ya juu Athanas Mdam alionyesha makeke yake jana
baada ya kufunga magoli matatu (hat-trick) katika mechi dhidi ya
Sierra-Leon ambapo Tanzania ilishinda 4-2 na kukata tiketi ya kushiriki
hatua inayofata ya michuano ya Mwaka ya kimataifa inayoandaliwa na
Airtel.
Mdamu
ambaye amedhiliisha kwamba yeye ni liungo muhimu katika michuano hii ,
alifunga magoli katika dakika ya 6, 48, 56 , Omari Hamisi ndiye
aliitimisha goli la nne la Tanzania katika dakika ya 60. Sierra-Leone
walipata magoli yao kupitia kwa Mohamed Mustapha katika dakika ya 8 na
Alimamy katika dakika ya 14.
Timu
ya wavulana ya Tanzania itacheza mechi ya robo fainali na Madagascar leo
wakati wasichana watacheza na Democratic Republic of Congo. Timu ya
wavulana itakosa huduma ya mpikaji mabao Athanas Mdamu ambaye yupo
majeruhi.
Mshambuliaji
hatari Athanas Mdamu ametoa mchango mkubwa sana katika timu mpka
kufikia hatua ya mtoano . Amefunga goli kwa kila mechi , dhidi ya Ghana
na Zambia. “ Tutamkosa ila tutapigana mpaka mwisho kuakikisha tuanshinda
mechi zote.”Alisema naodha wa timu Thomas Chndeka .
Timu
nyingine zilizofanikiwa kutinga katika hatua ya robo fainali kwa upande
wa wavulana ni mabingwa watetezi Niger ,wenyeji Nigeria , Chad, Malawi,
Madagascar, Zambia, na Congo. Na kwa upande wa wasichana ni mabingwa
watetezi Ghana , Nigeria , Chad, Kenya , Uganda , Malawi and DRC.
Mashindano
ya kimataifa ya Airtel Rising Stars ni mpango wenye lengo la kuchangia
maendeleo ya mpira wa miguu barani Afrika. Pia vijana wanapata fulsa ya
kuonyesha uwezo na vipaji vyao katika medani ya soka.
0 maoni:
Post a Comment