Friday, September 20, 2013

SPAIN YAMCHEKA MOURINHO KWA VIPIGO CHELSEA!

 
Kutokana na vipigo mfululizo kwa Jose Mourinho na Chelsea yake vimepokewa kwa vicheko na wapinzani wake huko Spain ambako Meneja huyo wa Chelsea aliishi na Real Madrid na kujitumbukiza katika utata na migogoro kibao.

Wakati Klabu yake ya zamani Real Madrid ikisheherekea ushindi wa Ugenini wa Bao 6-1 walipoitwanga Galatasaray huko Uturuki hapo Jumanne kwenye Mechi ya Makundi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, Jose Mourinho alijikuta akiangukia pua kwa kubandikwa Bao 2-1 na FC Basel kwenye Mashindano hayo hayo Siku ya Jumatano tena Uwanjani kwao Stamford Bridge.

Na hicho kilikuwa kipigo cha pili mfululizo kwa Jose Mourinho ambae Wikiendi iliyopita alibutuliwa Bao 1-0 na Everton kwenye Mechi ya Ligi Kuu England.
Hali hii imeleta vicheko huko Spain na baadhi ya kejeli ni Mabango: “Itachukua muda gani kabla hajambenchi Petr Cech!” na “Hana lolote bila Aitor Karanka!”
Mabango hayo yalikuwa yakimaanisha jinsi alivyompiga Benchi Nahodha na Kipa Nambari Wani wa Real na Spain, Iker Casillas, na ile tabia yake mambo yakiwa magumu kwake kumtuma Msaidizi wake Aitor Karanka kuongea na Wanahabari.

Lakini huko Nou Camp, kwa watani wa Mourinho alipokuwa Real, Mchezaji wa Barcelona, Gerrard Pique, ambae alifunga Bao moja wakati Timu yao inaichapa Ajax 4-0 kwenye UCL, aligusia kichapo cha Chelsea kwa kusema: “Kwenye Makundi ni lazima ukwepa kushangazwa! Chelsea, kufungwa na Basel Nyumbani, ni mfano huo na hilo linaleta mambo magumu.”

Jumatano 18 Sep 2013
FC Schalke 3 FC Steaua Bucureşti 0
Chelsea 1 FC Basel 2
Olympique de Marseille 1 Arsenal 2
SSC Napoli 2 Borussia Dortmund 1
FK Austria Wien 0 FC Porto 1
Club Atlético de Madrid 3 Football Club Zenit 1
AC Milan 2 Celtic FC 0
FC Barcelona 4 AFC Ajax 0


0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU