Afisa ushirika wa mkoa wa Iringa, John Kiteve wa (wa pili kulia)
akimkabidhi kikombe nahodha wa klabu ya Garden, Said amaohamed, mara baada ya
kuibuka mabingwa katika fainali za mashingano ya Safari Pool Taifa ngazi ya
mkoa yaliyomalizika mwishoni mwa wiki mkoani humo.Kulia ni Meneja mauzo wa Mkoa
wa Iringa, Philipo Kabecha na Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo.
Afisa
ushirika wa mkoa wa Iringa, John Kiteve(kulia) akimkabidhi kitita cha fedha
taslimu shilingi 700,000/= nahodha wa klabu ya Garden , Said Mohamed mara baada ya kuibuka mabingwa katika fainali za
mashingano ya Safari Pool Taifa ngazi ya mkoa yaliyomalizika mwishoni mwa wiki
mkoani humo.Kulia ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo.
Kamanda wa
Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani(wa pili kushoto) akimkabidhi nahodha
wa timu ya Royal Zambezi, Emmanuel Joram, kitita cha fedha taslimu shilingi
700,000/= mara baada ya kuibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Safari
Pool Taifa ngazi ya mkoa yaliyomalizika mwishoni mwa wiki mkoani humo.
MIKOA ya
Iringa, Mbeya na Dodoma hatimaye
imehitimisha fainali za mashindano ya Safari Pool Taifa ngazi ya mikoa na
kupata mabingwa wataowakilisha mikoa hiyo kwenye fainali za kitaifa zinazotarajiwa
kufanyika mkoani Morogoro.
Mkoa wa
Iringa upande wa timu,klabu ya Garden
ilifanikiwa kutwaa ubingwa kwa kuifunga klabu ya Ngija Masters 13-9 hivyo kuzawadiwa
kitita cha fedha taslimu shilingi 700,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha
mkoa wa Iringa kwenye fainali za kitaifa mkoani Morogoro
Upande wa
mchezaji mmoja mmoja wanaume(Singles), Goodlover Ntalande kutoka klabu ya
Garden alifanikiwa kutwaa ubingwa wa mkoa kwa kumfunga Emmanuel Joseph 5-2,na
hivyo kujinyakulia zawadi ya fedha taslimu shilingi 350,000/= pamoja na
kuwakilisha mkoa katika fainali za kitaifa mkoani Morogoro.
Upande wa
mchezaji mmoja mmoja wanawake, Naomi Ngede kutoka klabu ya Garden alitwaa
ubingwa kwa kumfunga Anna Elly 3-1, na kuzawadiwa fedha taslimu shilingi
250,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha mkoa wa Iringa kwenye fainali za
kitaifa mkoani Morogoro.
Mkoa wa Dodoma,klabu
ya Atlantic ilifanikiwa kutwaa
ubingwa hivyo kwa kuifunga klabu ya
Frolida na hivyo kuzawadiwa kitita cha fedha taslimu shilingi 700,000/= pamoja
na tiketi ya kuwakilisha mkoa wa Dodoma kwenye fainali za kitaifa mkoani Morogoro.
Upande wa
mchezaji mmoja mmoja wanaume(Singles), Mohamed Idd alifanikiwa kutwaa ubingwa
wa mkoa kwa kumfunga Ramadhani Issa,na hivyo kujinyakulia zawadi ya fedha
taslimu shilingi 350,000/= pamoja na kuwakilisha mkoa katika fainali za kitaifa
mkoani Morogoro.
Upande wa
mchezaji mmoja mmoja wanawake, Zainabu Salum alitwaa ubingwa kwa kumfunga Monica
Siimule, na kuzawadiwa fedha taslimu shilingi 250,000/= pamoja na tiketi ya
kuwakilisha mkoa kwenye fainali za kitaifa mkoani Morogoro.
Mkoa wa Mbeya,klabu
ya Royal Zambezi ilifanikiwa kutwaa
ubingwa kwa kuifunga klabu ya Shooters 13-2,na hivyo kuzwadiwa kitita cha fedha taslimu
shilingi 700,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha mkoa wa Mbeya kwenye fainali
za kitaifa mkoani Morogoro
Upande wa
mchezaji mmoja mmoja wanaume(Singles), Daniel Mbaga kutoka klabu ya Royal class
alifanikiwa kutwaa ubingwa wa mkoa kwa kumfunga Gibson Godwin 4-2,na hivyo
kujinyakulia zawadi ya fedha taslimu shilingi 350,000/= pamoja na kuwakilisha
mkoa wa Mbeya katika fainali za kitaifa mkoani Morogoro.
Upande wa
mchezaji mmoja mmoja wanawake, Rachel Richard kutoka klabu ya Kontena Tunduma
alitwaa ubingwa kwa kumfunga bingwa wa mwaka jana, Betty Sanga 3-2, na
kuzawadiwa fedha taslimu shilingi 250,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha
mkoa kwenye fainali za kitaifa mkoani
Morogoro.
Akizungumza
na wachezaji pamoja na wakazi wa Mbeya,Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscar
Shelukindo aliipongeza mikoa yote 17, kwa kumaliza vyema fainali za mashindano
hayo ngazi ya mikoa na hivyo kuviomba vilabu kujiaandaa kwa kwa muda uliobaki
kwa fainali ya kitaifa.
Shelukindo
aliisisitiza nidhamu katika mchezo ndio siri ya kila kitu katika mafanikio
mbele ya safari huko wanakoelekea kwenye fainali za kitaifa.Vilabu 17 kutoka
mikoa 17 vinatarajia kuchuana mkoani Morogoro na mwisho tutapata bingwa wa
Safari National Pool Championship 2013.
Fainali za
kitaifa zinatarajiwa kufanyika katika Mkoa wa Morogoro kuanzia Septemba 19 hadi
23,mwaka huu.
0 maoni:
Post a Comment