Bondia wa ngumi za kulipwa nchini karama nyilawila ambaye
alishawahi kuubeba ubingwa wa dunia wa WBF
–middle weight kwa kumpiga kreshnik qato
Wa Czech republic, katika ukumbi wa Sparta arena, plaque na kutwaa ubingwa huo ambao una hadhi kama aliokuwa nao francis
cheka kwa sasa, ambao baadae aliupoteza ubingwa huo kwa kutoutetea kutokana na
kukosa wadhamini wa kumsaidia kuutetea ubingwa wake huo, na kushawishika
kucheza na francis cheka katika pambano
alilopoteza na kukaa kimya muda mrefu bila kucheza pambano la ndani ya nchi.
Karama anategemea kupanda ulingoni tena tarehe 20 ya mwezi wa kumi katika ukumbi
wa ccm mwinjuma.Mwananyamala kuzipiga na
sado philemon katika pambano lililoandaliwa na bigright promotion.akilizungumzia pambano hilo
Ibrahim kamwe anaeleza kuwa maandalizi mpaka sasa yanaenda vizuri pindi yapo
katika mazingira magumu kwa wale watakaocheza utangulizi wanajiandaa kiukataukata
kwa ajili ya pambano hilo ambalo litakuwa na mapambano mengi ya utangulizi,
ukizingatia hatujapata mdhamini wa kudhamini pambano hili ili liwe katika ubora
unaotakiwa , lakini tunapambana na tutajitahidi pambano lifanyike vema tuwatie moyo hawa
mabondia wanaochipukia na kuusimamisha vizuri mchezo wetu wa masumbwi.Karama na
mwenzie philemon wameshasaini makubaliano ya mchezo huo na wapo katika hali
nzuri ya kimchezo.
0 maoni:
Post a Comment