Wednesday, September 4, 2013

POOL IRINGA

 Diwani wa Kata ya Kitanzini Mkoani Iringa,Madam Jesca Msavatangu(wa pili kushoto) akiwa kwenye maadamano na wachezaji wa Safari Pool Taifa ngazi ya mkoa wakelekea katika Hospitali ya Rufaa ya Manispaa ya Iringa  kutoa msaada wa vitu mbalimbali kabla ya kuanza mashindano hayo
 Diwani wa Kata ya Kitanzini Mkoani Iringa,Madam Jesca Msavatangu(kushoto) akimkabidhi Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali ya Manispaa ya Iringa, Rustila Tung’ombe  baadhi ya vitu walivyotoa msaada  katika Hospitali hiyo ambavyo ni pamoja na Sindano,Cloves,Sabuni na Machungwa kabla ya kuanza kwa mashindano ya  Safari Pool Taifa ngazi ya mkoa

 Diwani wa Kata ya Kitanzini Mkoani Iringa,Madam Jesca Msavatangu(katikati) akicheza pool kuashilia uzinduzi wa fainali za mashindano ya Safari Pool ngazi ya mkoa  yanayofanyika katika Ukumbi wa Olfare mkoani humo

Mchezaji wa kike wa Pool wa mkoa wa Iringa, akimkabidhi mama na moto zawadi ya Sabuni na machungwa kama pole wakati vilabu vya mkoa wa iringa vilipokwenda kutoa pole  na vifaa mbalimbali kwa wagongwa kabla ya kuanza kwa fainali za mashindano ya Safari Pool ngazi ya mkoa yalioanza jana mkoani humo

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU