Tuesday, September 24, 2013

SERIKALI YAUNGA MKONO REDIO ZA KIJAMII KATIKA KUHAMASISHA AMANI NA DEMOKRASIA KUELEKEA UCHAGUZI 2015

IMG_6499
Mkurugenzi wa Uvinza Fm Ayubu Kalufya akimtambulisha Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mwl. Khadija Nyembo kwa Meneja wa Mradi wa Demokrasia na Amani kutoka UNESCO Courtney Ivins mara baada ya kuwasili kwenye halfa ya kuzindua Mradi Wa UNESCO – UNDP wa kuhamasisha Amani katika mchakato wa kukuza Demokrasia katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mwaka 2015 uliofanyika kwenye Kituo tarajiwa cha Redio ya Jamii Uvinza Fm Wilayani Uvinza.
IMG_6502
Mwenyekiti wa Bodi ya Uvinza Fm Nuru Kalufya (wa pili kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mwl. Khadija Nyembo mara baada ya kuwasili.
IMG_6561
Mkurugenzi wa Uvinza Fm Ayubu Kalufya akitambulisha meza kuu kwa wageni waalikwa wakati wa hafla ya kuzindua mradi wa UNESCO-UNDP wa kuhamasisha Amani katika mchakato wa kukuza Demokrasia katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mwaka 2015.
IMG_6603
Meneja wa Airtel mkoani Kigoma Philip Nkupama akiwasalimia wageni waalikwa (hawapo pichani) kwenye hafla ya uzinduzi wa mradi huo uliofanyika kwenye kituo cha vijana Uvinza mkoani Kigoma.
IMG_6670
Mwenyekiti wa Bodi ya Uvinza Fm Nuru Kalufya akiwasalimia wageni waalikwa kwenye uzinduzi huo.
IMG_6598
Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mwl. Khadija Nyembo akiteta jambo na Mtaalamu mhandisi wa mitambo na mafunzo ya awali kwa watangazaji wa redio Uvinza Fm kutoka nchini Aurstralia Bw. Rukmin Wijemanne
IMG_6718
Mkuu wa Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma Mwl. Khadija Nyembo akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya wakati akizundua mradi wa UNESCO-UNDP wa kuhamasisha Amani katika mchakato wa kukuza Demokrasia katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mwaka 2015 uliofanyika kwenye Kituo tarajiwa cha Redio ya Jamii Uvinza Fm Wilayani Uvinza mkoani Kigoma.
IMG_6585
Sehemu ya wageni waalikwa na waandishi wa habari watarajiwa wa Redio Uvinza Fm wakimsikiliza mgeni rasmi.
IMG_6785
Meneja wa Airtel mkoani Kigoma Philip Nkupama akizungumza nia yao ya kutoa ufadhili kwa Redio Uvinza Fm kurusha matangazo yao kupitia minara ya Airtel ambapo pia amesema lengo lao ni kusaidia jamii zilizo na changamoto mbalimbali ikiwemo za mila potofu, Elimu duni, Ukeketwaji, imani za kishirikina, maendeleo duni , ukandamizaji wa Wanawake na Watoto na changamoto nyingine nyingi.
Ameongeza kuwa kupitia mradi wa Redio Jamii, Jamii itafikishiwa taarifa zote pamoja na kupambana na changamoto mbalimbali nchini kwenye Siasa, Uchumi na Utamaduni na wakati huo huo kuiongezea jamii ufahamu kuhusu hali ya mwelekeo wa nchi yao kwa ujumla.
IMG_6805
Kikundi cha kinamama cha Uhamasishaji cha Warumba wilayani Uvinza kikitoa burudani wakati wa hafla hiyo.
IMG_6797
Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mwl. Khadija Nyembo (wa tatu kushoto) akishiriki kucheza ngoma za asili na kinamama wa kikundi cha uhamasishaji wilayani humo Warumba wakati wa hafla hiyo.
IMG_6866
Mkufunzi wa Redio za Jamii kutoka Unesco Mama Rose Haji Mwalimu akifafanua jambo mbele ya mgeni rasmi jinsi atakavyoendesha mafunzo hayo kwa waandishi na watangazaji watarajiwa wa Redio Uvinza Fm ambapo masomo hayo yatagusa nyanja mbalimbali ikiwemo habari ni nini, mbinu za kuibua habari, habari na jinsia na kuelimisha jamii. Watajifunza pia jinsi ya kuhariri habari, miundo mbalimbali ya vipindi kwa mujibu wa mwongozo mamlaka ya mawasiliano Tanzania-TCRA,’
IMG_6851
Meneja wa Mradi wa Demokrasia na Amani kutoka Unesco Courtney Ivins akifafanua jinsi mradi huo utakavyotekelezwa na Redio za Jamii nchini kuelekea uchaguzi mwaka 2015.
IMG_6899
Kundi la Black and White kutoka wilayani Uvinza likitoa burudani ikiwa ni fundisho kwa mambo yanayojitokeza wilayani humo lakini hayana mahali pa kusemewa, Redio Uvinza itasaidia kukomesha matukio kama hayo ya ukabaji.
IMG_6730
Baadhi ya madiwani wa Wilaya ya Uvinza waliohudhuria uiznduzi huo.
IMG_7034
Baadhi ya waandishi wa Redio Uvinza Fm wakisaidiana kubeba mitambo mipya ya Redio ya Jamii Uvinza Fm iliyotolewa na shirika la UNESCO kwa kushirikiana na UNDP.
IMG_7051
Mtaalamu mhandisi wa mitambo na mafunzo ya awali kwa watangazaji wa redio Uvinza Fm Bw. Rukmin Wijemanne akihakiki mitambo ya Redio hiyo kama imekamilika tayari kuifunga. Kulia ni Meneja wa mradi wa DEP Courtney Ivins akikagua maboksi ya vifaa hivyo.
IMG_7018
Mkufunzi wa Redio za Jamii kutoka Unesco Mama Rose Haji Mwalimu, Meneja wa Airtel mkoani Kigoma Philip Nkupama wakiwa kwenye picha ya pamoja na waandishi na watangazaji watarajiwa wa Redio Uvinza Fm.
IMG_7045
Mkufunzi wa Redio za Jamii kutoka Unesco Mama Rose Haji Mwalimu akiagana na Meneja wa Airtel Mkoani Kigoma Philip Nkupama aliyeambatana na Mratibu wa Maendeleo ya Biashara wa Airtel mkoani Kigoma Bw. Samwel Lumanyisa mara baada ya kuhitimisha hafla ya uzinduzi wa mradi huo.

Serikali inakaribisha miradi ya kuhamasisha amani katika mchakato wa kukuza demokrasia katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mwaka 2015 inayozingatia habari za uhakika na maadili ya kiafrika kupitia radio za kijamii.
Akisoma hotuba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Mkuu wa Wilaya ya Uvinza, Bi Khadija Nyembo kwenye hafla ya uzinduzi wa mradi wa shirika la umoja wa mataifa la elimu, sayansi na utamaduni (UNESCO) wakishirikiana na shirika lingine la umoja wa mataifa la programu za maendeleo (UNDP) amesema mradi huu wa amani unahamasisha jamii umuhimu wa amani ili kukuza demokrasia nchini.

“mafunzo ya mafundi mitambo yanayoendeshwa na mtaalamu mhandisi wa mitambo kutoka Australia pamoja na mafunzo ya awali kwa watangazaji wa redio kituoni hapa na wale maripota wa kujitolea kutoka baadhi ya vijiji na kata ambazo redio hii ya Uvinza FM itasikika, ni mafanikio makubwa kwa maendeleo ya wilaya ya Uvinza na mkoa wa Kigoma kwa ujumla,” amesema Kiongozi huyo.
Amesema wanahabari watakaoshiriki katika warsha hii ya siku tano watajifunza na kufanya mazoezi katika mada za kitaaluma pamoja na kanuni za maadili katika kutafuta na kuripoti habari.

“watajifunza habari ni nini, mbinu za kuibua habari, habari na jinsia na kuelimisha jamii. Watajifunza pia jinsi ya kuhariri habari, miundo mbalimbali ya vipindi kwa mujibu wa mwongozo mamlaka ya mawasiliano Tanzania-TCRA,’ amefafanua.
Bi Nyembo amesema Kampuni ya simu za viganjani ya Airtel imetoa msaada kwa kuruhusu minara yake itumike kurushia matangazo kutoka kituo cha Uvinza FM Radio kwa upande mmoja na kwa upande mwingine wanashirikiana na serikali za mitaa katika kufanikisha mradi huo.

Amesema kitendo cha halmashauri ya wilaya ya Uvinza na halmashauri ya kijiji cha Uvinza kwa pamoja kutoa sehemu moja ya jengo la vijana kwa ajili ya Uvinza FM Radio ni jambo la kuigwa katika jamii kwa ujumla.
“Kwa niaba ya serikali yote hapa mkoani kwa ujumla natoa pongezi zangu za dhati kwa wadau hao wote waliowezesha na watakaowezesha ukamilishaji wa mtambo huu na pia kuendeshwa kwa mradi huu wa UNESCO-UNDP wa uhamasishaji wa amani katika mchakato wa demokrasia kuelekea uchaguzi 2015.

“Kwa mujibu wa UNESCO mradi huu utazihusisha redio 26 zilizoko Tanzania bara na visiwani. Kati ya redio hizo tatu mpya zitajengwa na kuanzishwa Micheweni Pemba, Tumbatu Unguja ikiwemo Uvinza FM redio jamii Tanzania bara. Ni jambo la kujivunia,”.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU