Baraza la wazee wa YANGA limesema halimtambui katibu
mpya wa YANGA aliyeletwa na kumuondoa
katibu aliyekuwepo RAWLENCE MWALUSAKO kwani viongozi waliomleta
wamekiuka katiba ya YANGA.
IBRAHIM AKILIMALI ambaye ni katibu wa baraza la
wazee amesema wamepata taarifa za kuondolewa kwa katibu wa YANGA wa zamani
RAWLENCE MWALUSAKO jambo ambalo wamepinga vikali
Baadhi ya wazee wa YANGA wamesema walikutana na
katibu mpya klabuni katika mahojiano naye akashindwa kumtaja mtu aliyemleta kufanya
kazi .
Baraza la wazee YANGA limesema halikatai kuletwa
viongozi wapya bali uongozi wa YANGA ufuate taaratibu za katiba ya YANGA
inavyotaka ikiwemo kutoa taarifa kwa kamati mbalimbali za YANGA ili zifahamu
mabadiliko katika uongozi.
Wamesema katiba ya YANGA inataka kiongozi yoyote awe
ni mwanachama halali wa YANGA na anafahamu taratibu za YANGA ndipo atafanya
kazi
0 maoni:
Post a Comment