Thursday, October 3, 2013

MAN CITY HOI KOMBE LA UEFA


MECHI za Pili za Makundi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI,UCL, zimekamilika jana usiku  kwa Mabingwa Watetezi Bayern Munich kushusha kichapo cha Bao 3-1 Ugenini Uwanja wa Etihad kwa Wenyeji wao Man City huku .

BAYERN MUNICH ilinza kupata bao la kuongoza kupitia kwa mshabuliaji wao RIBÉRY dakika ya saba ya mchezo huku ngome ya MAN CITY ikionekana kuhelemewa muda waote.

Kwa kicheza kwa kujiamini zaidi BAYERN MUNICH alifunga bao pili dakika ya 56 kupitia kwa mchezaji  Müller huko kapu la magoli likifungwa kwa mchezaji  Robben alifunga dakika ya 59.

MANCHESTER CITY wakiwa wanyonge nyumbani katika uwanja wao wa ETIHAD walifunga bao la kufutia machozi dakika 79 kupitia kwa mchezaji  Negredo .

Naye bingwa mtetezi wa ligi kuu ENGLAND MANCHESTER UNITED alijikuta akitoka sare ya kufungana bao moja kwa moja na FC SHAKHTAR DONETSK
Krosi ya Marouane Fellaini ilimpita Beki wa Shakhtar Rakitskiy na Danny Welbeck kuchomoka na kuunganisha na kuipa Bao la kwanza katika Dakika ya 18.

Kipindi cha Pili, Shakhtar walikuja juu na kusawazisha kwa Bao la Dakika ya 76 la Taison.

Ryan Giggs aliingizwa Kipindi cha Pili kuchukua nafasi ya Fellaini na kumfanya aweke Rekodi ya kuwa Mchezaji pekee aliecheza Mechi nyingi za uefa  kwa kucheza Mechi 145 na kumpita Raul aliecheza Mechi 144.

Man United wanaongoza Kundi A wakiwa na Pointi 4 sawa na Shakhtar lakini wamewazidi kwa ubora wa Magoli.

Hegeler aliifungia Bayer Leverkusen Bao la Dakika ya 90 na kuwapa ushindi wa Bao 2-1 dhidi ya Real Sociedad.

Simon Rolfes alifunga Bao katika Dakika ya 45 na kuifanya Bayer Leverkusen iende Mapumziko ikiwa mbele kwa Bao 1-0.

Kipindi cha Pili Carlos Alberto Vela alikosa Penati lakini akauwahi Mpira huo na kuisawazishia Real Sociedad.

Nayo timu ya ya REAL MADRID iliibuka na ushindi wa mabao manne kwa bila dhidi ya FC COPENHAGENI .

Bao 2 za Cristiano Ronaldo na 2 za Angel Di Maria zimewapa Real Madrid ushindi wa Bao 4-0 Uwanjani kwao Santiago Bernabeu walipocheza na FC Copenhagen.

Wakiwa kwao Juventus Arena, Mabingwa wa Italy Juventus walijikuta wakati wa Haftaimu wako nyuma kwa Bao la Didier Drogba la Dakika ya 36 lakini Kipindi cha Pili walisawazisha kwa Bao la Penati ya Arturo Vidal ya Dakika ya 78 na Fabio Quagliarella kuongeza Bao la Pili Dakika ya 87.

Galatasaray walisawazisha katika Dakika ya 88 kwa Bao la Umut Bulut na kuifanya Gemu imalizike 2-2.

Olympiakos iliibuka kidedea kwa ushindi wa bao tatu kwa bila dhidi ya Anderlecht huku PSG ikiinyuka BENFICA mabao matatu kwa bilia
Nayo timu ya CSKA Moscow  ikaifunga Viktoria Pilsen mabao matatu kwa mawili

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU