Bingwa wa
Afrika wa mchezo wa Pool kutoka Tanzania, Patrick Nyangusi (kushoto) akiwa na
mpinzani wake, Vishen Jagdev kutoka Afrika Kusini kabla ya kuanza mchezo wa
fainali uliofanyika jijini Blantyre nchini Malawi mwishoni mwa wiki.
Bingwa wa
Afrika wa mchezo wa Pool kutoka Tanzania, Patrick Nyangusi akicheza dhidi ya
mpinzani wake, Vishen Jagdev kutoka Afrika Kusini (hayupo pichani) wakati wa
mchezo wa fainali uliofanyika Blantyre Malawi mwishoni mwa wiki.
Wachezaji na
mashabiki wa timu ya Taifa ya Safari Pool ya nchini Tanzania wakiwa wamembeba
mchezaji,Patrick Nyangusi mara baada ya kutwaa ubingwa wa Afrika wa mchezaji
mmoja mmoja (Singles) kwa kumfunga Vishen Jagdev wa Afrika Kusini 6-4,katika
mchezo uliofanyika Blantyre Malawi mwishoni mwa wiki.
Wachezaji na
mashabiki wa timu ya Safari Pool kutoka Tanzania wakishandilia na mchezaji
Patrick Nyangusi mara baada ya kutwaa ubingwa wa mchezaji mmoja mmoja (Singles)
Afrika uliofanyika Blantyre Malawi mwishoni mwa wiki.
Wachezaji wa
timu ya Taifa ya Safari Pool ya Tanzania wakiwa na medali zao za Fedha mara
baada ya kutunukiwa kwa kupata nafasi ya tatu katika mashindano ya Pool Afrika
yaliyofanyika jijini Blantyre Malawi mwishoni mwa wiki
Mgeni
rasmi,Mjumbe wa Baraza la Michezo Nchini Malawi, Sharaf Pinto(wa pili kushoto)
akiwa na mabingwa wa Singles(mchezaji mmoja mmoja).Kutoka kulia ni mshindi wa
tatu kutoka Zambia, Moses Mofya,mshindi wa pili kutoka Afrika Kusini, Vishen
Jagdev na Bingwa gwa Afrika kutoka Tanzania, Patrick Nyangusi wakiwa katika
picha ya pamoja mara baada ya kuwakabidhi medali zao Blantyre Malawi mwishoni
mwa wiki.
Mabingwa wa
Afrika wa mchezo wa pool wakiwa katika
picha nya pamoja.Kutoka kushoto ni Bingwa wa Afrika kutoka Tnzania, Patrick
Nyangusi,mshindi wa pili kutoka Afrika Kusini, Vishen Jagdev na mshindi wa tatu
kutoka Zambia, Moses Mofya mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao jijini Blantyre
Malawi mwishoni mwa wiki.
0 maoni:
Post a Comment