Monday, October 28, 2013

YANGA, MGAMBO KUUMANA UWANJA WA TAIFA VPL

 
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inakamilisha  raundi ya kumi na moja kesho (Oktoba 29 mwaka huu) kwa mechi tatu huku Yanga ikiwa mwenyeji wa Mgambo Shooting kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Mbeya City na Tanzania Prisons. Rhino Rangers na JKT Ruvu zitacheza katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.

Raundi ya 12 ya ligi hiyo itaanza Oktoba 31 mwaka huu kwa mechi kati ya Simba na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Novemba Mosi mwaka huu kutakuwa na mechi kati ya Yanga na JKT Ruvu kwenye uwanja huo huo.

Novemba 2 mwaka huu kutakuwa na mechi nne; Mgambo Shooting na Coastal Union (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Tanzania Prisons na Oljoro JKT (Uwanja wa Sokoine, Mbeya), Azam na Ruvu Shooting (Azam Complex, Dar es Salaam), na Mtibwa Sugar na Rhino Rangers (Uwanja wa Manungu, Morogoro).

Raundi hiyo itakamilika Novemba 3 mwaka huu kwa mechi moja ambapo Mbeya City itakuwa mwenyeji wa Ashanti United kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Mechi za kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo zitachezwa Novemba 6 na 7 mwaka huu. Novemba 6 ni JKT Ruvu vs Coastal Union, Ashani United vs Simba, Kagera Sugar vs Mgambo Shooting, Rhino Rangers vs Tanzania Prisons na Ruvu Shooting vs Mtibwa Sugar.

Novemba 7 mwaka huu, Azam itacheza na Mbeya City wakati Yanga itacheza na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

EL MAAMRY KUONGOZA BODI YA TFF
Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) umemteua Said Hamad El Maamry kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ambayo kazi yake kubwa ni kusimamia mali za shirikisho.

El Maamry ambaye kitaaluma ni mwanasheria na Mwenyekiti wa zamani wa TFF wakati huo ikiwa Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (FAT) ataongoza bodi hiyo yenye jumla ya wajumbe watano.

Wajumbe wengine wa bodi hiyo ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera ambaye anakuwa Makamu Mwenyekiti, Dk. Ramadhan Dau, Mohamed Abdulaziz na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Stephen Mashishanga.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU