Meneja
masoko wa Kampuni ya Samsung nchini, Sylivester Manyara (kushoto),Msimamizi
mwandamizi wa Bahati na sibu ya Taifa, Emmanuel Mdaki na Mratibu wa Programu za
Samsung, Lawrence Andrew wakichezesha droo ya mwezi kwa wateja wa bidhaa za Kampuni
hiyo Mwenge Dar es Salaam jana.
Meneja
masoko wa Kampuni ya Samsung nchini, Sylivester Manyara (kushoto),Msimamizi
mwandamizi wa Bahati na sibu ya Taifa, Emmanuel Mdaki na Mratibu wa Programu za
Samsung, Lawrence Andrew wakimpigia mteja aliyeshinda kwenye droo ya mwezi kwa
wateja wa bidhaa za Kampuni hiyo Mwenge Dar es Salaam jana.
Meneja
masoko wa Kampuni ya Samsung nchini, Sylivester Manyara(wa tatu kushoto)
akiwaonyesha baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam namana ya droo inavyochezesha na washindi
wanavyopatikana wakati wa kuchezesha droo ya mwezi iliyochezeshwa Mwenge Dar es
Salaam jana.
Kwa mara nyingine
tena Kampuni ya Samsung Tanzania imechezesha droo ya mfumo wake wa
“E-Warranty”, washindi walitangazwa katika hafla iliyoandaliwa katika Stendi
Kuu ya Mwenge, jijini Dar es Salaam. Mfumo huu wa “E-Warranty ni mbinu
inayotumiwa na Kampuni ya Samsung kama jinsi ya kukumbana na bidhaa feki
zinazopatikana kwenye soko la Tanzania.
Mfumo huo wa
e-warranty unawasaidia wateja kujua kama simu ya Samsung ni halali au ni feki.
Wateja wanapaswa kusajali simu zao pale wanapozinunua na hivyo kupata dhamana
ya miezi 24.
Meneja Mkuu wa Samsung Tanzania, Bwana Kishor Kumar akizungumuza na waandishi wa habari alisema
“Mfumo wa E-Warranty imeonyesha kwamba ni mbinu bora zaidi dhidi ya kukumbana
na bidhaa feki kwani wateja wengi wanasajili simu zao. Tunawahimiza wateja
wetu waendele kutuunga mkono kwa kununu
bidhaa bora na kuzisajili na hivyo kupata nafasi ya kujishindia bidhaa kabambe
za Samsung katika droo zetu”.
Washindi wanaweza
kushinda zawadi 1 kati ya hizi 10: Televisheni 1 aina ya LED ya inchi 32,
laptop 1, Kamera 3, home theatre 3 na simu 2 aina ya Galaxy Grand.
Bwana Kumar
aliendelea kusema “ Licha na kujua kama simu mteja anayotaka kununua ni bora au
feki, mfumo wa e-warranty unawasiadia wateja kujua kama simu hiyo inadhama ya
miezi 24, kama simu hiyo inatafutwa au imeibiwa na kama simu hiyo ni mpya au
imeshatumika”.
Kujua kama simu ni
halali, mteja anatakiwa kufuta maelekezo yafuatayo: Tuma ujumbe na neno ‘Check’
ikifuatiwa na alama ya nyota (*) kisha namba ya IMEI, ikifuatiwa
na alama ya reli (#) na kutuma kwa namba ‘15685’. Ujumbe unatumwa
moja kwa moja kuelezea hadhi ya simu hiyo ya Samsung.
“Mfumo huu wa
e-warranty ulianzishwa haswa kukabiliana na changamoto moto inayoikumba soko la
simu za mkononi huku Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla, ambapo kuna simu
nyingi ni za bandia, za wizi, zilizotumika na simu ambazo hazina dhamana”,
alisema Bwana, Kumar.
Bwana Kumar
alimaliza kwa kusema ‘ili kuboresha huduma zetu za mfumo wa e-warranty, wateja
watakaonunua simu aina ya Galaxy S 4 (iliyozinduliwa mwezi huu jijini Dar es
Salaam), watapata huduma mpya inayoitwa ADH. ADH (Accidental Damage from
Handling), ni huduma inayoilinda simu hiyo ya S 4 kutoka uharibifu kutokana na
matumizi ya kawaida’.
Ilikujiunga na
huduma ya ADH, wateja wanatakiwa kujisajili na mfumo wa e-warranty na usajili
untakiwa kufanywa ndani ya siku 30 tangu kununuliwa kwa simu. Athari ya
kutokujiunga na mfumo wa e-warranty kwa muda unaotakikana ni kwamba simu hiyo
ya S4 haitaweza kutengenezwa kwa bure pale ambapo itaharibika.
0 maoni:
Post a Comment