MABINGWA wa Tanzania Bara, Yanga, itabidi wajilaumu sana maana walishawaweka Simba pabaya
sana kwa kumudu kuongoza Bao 3-0 hadi Haftaimu Uwanja wa Taifa
Jijini Dar es Salaam lakini Simba waliibuka Kipindi cha Pili na
kusawazisha Bao zote na Mechi hii ya VPL, Ligi Kuu Vodacom kumalizika
kwa Sare ya Bao 3-3.
MAGOLI:
Simba 3
- Betram Mombeki Dakika ya 54
-Joseph Owino 58
- Kaze Gilbert 85
Yanga 3
-Mrisho Ngassa Dakika ya 15
-Hamis Kiiza 36
-Hamisi Kiiza 45
Ni wazi uamuzi wa Kocha wa Simba
Abdallah Kibaden kubadilisha Kikosi chake na kuwaingiza Said Ndemla na
William Lucian badala ya Haruna Chanongo na Abdulhalim Humud mwanzoni
mwa Kipindi cha Pili kuliwasaidia Simba kupata Sare hii.
0 maoni:
Post a Comment