Thursday, November 7, 2013

AIRTEL SHULE YETU YAFAGILIWA NA WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI ILULU -LINDI ,

 Meneja masoko wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kanda ya kusini na mkoa wa Morogoro Aminata Keita akikabidhi baadhi ya Vitabu vilivyotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa Salma Hamisi ambaye ni mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Ilulu iliyopo mkoani Lindi. Airtel ilitoa vitabu  vyenye thamani ya shilingi Milioni tano kwa shule hiyo.
 Meneja masoko wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kanda ya kusini na mkoa wa Morogoro Aminata Keita akimkabidhi Bernard Swai ambaye ni mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Chalinze. Airtel ilitoa vitabu vyenye thamani ya shilingi milioni tano kwa shule hiyo.
 Meneja masoko wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kanda ya kusini na mkoa wa Morogoro Aminata Keita akimkabidhi Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule ya sekondari ya Chalinze iliyopo mkoani Pwani baadhi ya vitabu vilivyotolewa na Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa shule ya sekondari Chalinze. Wanaoshuhudia katikati ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Bw. Emmanuel Kahabi pamoja na msimamizi wa bodi ya shule hiyo Bw. Mzee Madeni.
Meneja masoko wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kanda ya kusini na mkoa wa Morogoro Aminata Keita akiwaelekeza jambo watoto wa shule ya sekondari Nanyamba iliyopo Mkoani Mtwara ikiwa ni muda mfupi baada ya kampuni ya mitandao ya simu za mkononi Airtel kukabidhi vitabu vyenye thamani ya shilingi milioni tano kwa shule hiyo ya sekondari.

Wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya Ilulu iliyoko wilayani Kilwa mkoani Lindi,wameishukuru kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kuwapatia msaada wa vitabu vya masomo ya sayansi vyenye thamani ya shilingi milioni tano.

Wakizungumza shuleni hapo mara baada ya kupokea msaada huo wanafunzi hao wamesema kwamba wanafunzi wasichana wanauwezo wa kusoma masomo ya sayansi na kufanya vizuri isipokuwa changamoto kubwa inayowakabili ni ukosefu wa maabara na vitabu.

Wanafunzi hao wameishukuru kampuni ya simu ya airtel na kusema kwamba hivi sasa watasoma kwa bidii masomo hayo ya sayansi kwani kukosekana kwa vitabu hivyo kulikuwa kunachangia kutofanya vizuri katika masomo hayo.

"Tumekua tunapata shida sana kujifunza masomo ya sayansi kwani hapa shuleni kwetu hakuna hata maktaba wala maabara kwa ajili ya masomo hayo," alisema Rehema Issa.
"Vitabu hivi vitatuwezesha kufaulu masomo yetu ya sayansi japo bado tunakabiwa na tatizo na maabara aliongeza Blandina Charles mwanafunzi wa kidato cha tatu shuleni hapo.
Meneja masoko wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kanda ya kusini na mkoa wa morogoro Aminata Keita, amesema msaada huo ni mchango wa airtel katika elimu hapa nchini.

Keita amesema zoezi hilo la kutoa vitabu vya masomo ya sayansi linaendelea katika shule 35 za sekondari hapa nchini ili kuwawezesha wanafunzi kufanya vizuri katika masomo ya sayansi.
"Kwetu sisi Airtel hii ni fahari kubwa kushirikiana na shule hii katika kukuza ufaulu hasa kupitia vitabu hivi vya kiada ambavyo ni vya masomo ya sayansi" alisisitiza Keita.
"Mpaka sasa tumezifikia shule nyingi sana na Ilulu secondary imepata fursa ya kupata msaa huu, nawasihi mvitumie vitabu hivi kwa manufaa yenu na wenzenu watakaosoma hapa," alimalizia Aminata

Utaratibu wa kusaidia elimu kupitia mpango wa shule yetu ulio chini ya kampuni ya simu za mkononi ya airtel unachangia ukuaji wa sekta ya elimu kupitia vitabu vya masomo ya sayansi.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU