Mke wa Mjumbe wa Tume
ya Mabadiliko ya Katiba, Dkt. Sengondo Mvungi, …(kulia) pamoja na marafiki
wakiomba dua leo (Alhamisi, Novemba 7, 2013) katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu
Nyerere dakika chache kabla na Dkt. Mvungi hajasafishwa kwenda Afrika Kusini kwa
matibabu zaidi. Kushoto ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Bw. James Mbatia. Dkt.
Mvungi alivamiwa na kujeruhiwa na watu nyumbani kwake Kibamba jijini Dar es
Salaam usiku wa kuamkia Jumapili, Novemba 3, 2013.
Dkt. Mugisha Clement
Mazoko wa Kitengo cha Mifupa Muhimbili (MOI) (kushoto), Katibu wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba Bw. Assaa Rashid (mwenye tai) na Mwenyekiti wa NCCR
Mageuzi Bw. James Mbatia (wa pili kulia) pamoja na ndugu na jamaa wa Mjumbe wa
Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dkt. Sengondo Mvungi wakiangalia wakati Mjumbe
huyo akipandishwa ndani ya ndege kusafirishwa kwenda Afrika Kusini kwa matibabu
zaidi. Dkt. Mvungi alivamiwa na kujeruhiwa na watu nyumbani kwake Kibamba
jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia Jumapili, Novemba 3, 2013.
Tume
ya Mabadiliko ya Katiba inapenda kuwafahamisha wananchi kuwa Mjumbe wake Dkt.
Sengondo Mvungi aliyekuwa akipata matibabu katika Kitengo cha Mifupa Muhimbili
(MOI) amesafirishwa leo (Alhamisi, Novemba 7, 2013) saa 5:45 asubuhi kwenda
nchini Afrika Kusini kwa uchunguzi na matibabu zaidi.
Akiwa
nchini Afrika Kusini, Dkt. Mvungi atapata matibabu katika Hospital ya Milpark
iliyopo jijini Johannesburg.
Itakumbukwa
kuwa Dkt. Mvungi alivamiwa nyumbani kwake Kibamba, wilaya ya Kinondoni jijini
Dar es Salaam na watu waliomjeruhi vibaya kichwani usiku wa kuamkia siku ya
Jumapili, Novemba 3, 2013. Tukio hilo la uvamizi linaendelea kuchunguzwa na
vyombo vya ulinzi na usalama nchini.
Tangu
siku alipojeruhiwa, Dkt. Mvungi alikuwa akipata matibabu katika Kitengo cha
Mifupa Muhimbili (MOI). Hata hivyo, Madaktari waliokuwa wakimtibu MOI,
walishauri afanyiwe uchunguzi na matibabu zaidi.
Dkt.
Mvungi ameondoka na ndege ya kukodi ya Shirika la Ndege la Flightlink na
ameambatana na Dkt. Mugisha Clement Mazoko kutoka MOI; Muuguzi Bi. Juliana
Moshi; na mtoto wa kaka yake Bw. Deogratias Mwarabu. Serikali inagharamia
gharama zote za matibabu ya Dkt. Mvungi.
Tume
inawaomba wananchi wote waendelee kumuombea kwa Mungu Dkt. Mvungi ili aweze
kurejea katika hali yake ya kawaida na hatimaye kuendelea majukumu yake.
0 maoni:
Post a Comment