Sunday, November 10, 2013

BancABC YASHIRIKIANA NA MEHATA KUSAIDIA WENYE MATATIZO YA UBONGO TANZANIA

Dokta, Stellah Mshana(kushoto) wa Chama cha Madaktari wa Magonjwa ya Ubongo Tanzania (MEHATA) wa Hospiti ya Korogwe Tanga, akizungumza na wafanyakazi wa BancABC walipotembela Hospitali hiyo kutoa msaada wakishirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afya ya Ubongo Duniani ambayo kitaifa yalifanyika Mkoani Tanga.

Chama cha Madaktari wa Magonjwa ya Ubongo Tanzania (MEHATA), kwa ushirikiano na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii iliandaa maadhimisho ya Siku ya Afya ya Ubongo Duniani ambayo kitaifa yalifanyika Mkoani Tanga.

Kilele cha mahadhimisho hayo ilikuwa ni tarehe 10 Oktoba 2013, ambapo BancABC pamoja na madaktari kutoka taasisi mbalimbali zinazojihusisha na afya ya Ubongo, walitembelea hospitali za Wilaya mkoani Tanga kuanzia tarehe 9 oktoba mpaka tarehe 10 oktoba 2013.

Lengo la ziara hiyo lilikuwa ni kutathmini Huduma za magonjwa yaambatanayo na afya ya Ubongo ambazo zinatolewa katika hospitali za Wilaya Mkoani humo. BancABC ilipata nafasi ya kutembelea hospitali za wilaya ya Bombo, Lushoto, na Korogwe. Lengo lingine likiwa ni kuwasaidia madaktari na wauguzi katika utoaji wa Huduma za afya kwa wagonjwa walio athirika zaidi na matatizo hayo. Pia, ziara hii iliambatana na kushughulikia ikiwa ni pamoja na kuyapatia ufumbuzi maswala yanayo pelekea kuzorota kwa utoaji wa huduma bora za afya kwa wagonjwa wa matatizo ya ubongo mkoani humo.

Ni faraja kubwa kwa BancABC kushiriki katika mchakato huu, kwani kundi la wagonjwa wa afya ya Ubongo, limesahaulika kwa kiasi na watu wengi katika jamii yetu. Ni muhimu kutambua kwamba matatizo ya afya ya ubongo, yanakuwa kwa kasi na hivyo BancABC wameona uhitaji wa kundi hili na hivyo kuamua kutoa mchango wao, kama mpango wa kurudhisha kwa jamii kutokana na biashara nzuri wanayofanya. BancABC inawahimiza na kuwasihi mashirika mengine na watu binafsi, kushiriki katika kuchangia kundi hili ili kuokoa nguvu kazi ya nchi yetu.
 


0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU