Raundi
 ya 12 ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) ambayo ipo katika raundi yake ya 12 
inaendelea kesho (Novemba 2 mwaka huu) kwa mechi nne zitakazochezwa 
katika miji minne tofauti.
Mgambo
 Shooting na Coastal Union zitaoneshana kazi kwenye Uwanja wa Mkwakwani 
jijini Tanga, Mbeya City na Ashanti United zitaumana kwenye Uwanja wa 
Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya, Azam na Ruvu Shooting (Azam Complex,
 Dar es Salaam), na Mtibwa Sugar na Rhino Rangers (Uwanja wa Manungu, 
Morogoro).
Raundi
 hiyo itakamilika Novemba 3 mwaka huu kwa mechi moja ambapo Tanzania 
Prisons itakuwa mwenyeji wa Oljoro kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya 
Sokoine jijini Mbeya.
Mechi
 za kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo zitachezwa Novemba 6 na 7
 mwaka huu. Novemba 6 ni JKT Ruvu vs Coastal Union, Ashanti United vs 
Simba, Kagera Sugar vs Mgambo Shooting, na Ruvu Shooting vs Mtibwa 
Sugar.
Novemba
 7 mwaka huu, Azam itacheza na Mbeya City, Yanga itacheza na Oljoro JKT 
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Rhino itakuwa mwenyeji wa 
Tanzania Prisons.
MECHI YA SIMBA, KAGERA YAINGIZA MIL 32
Mechi
 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Kagera iliyochezwa jana (Oktoba
 31 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 32,726,000.
Washabiki
 waliohudhuria mechi hiyo namba 81 iliyomalizika kwa timu hizo kutoka 
sare ya bao 1-1 walikuwa 5,541 ambapo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 
8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.
Mgawo
 wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; Kodi ya Ongezeko la Thamani 
(VAT) sh. 4,992,101.69, gharama za kuchapa tiketi sh. 3,183,890 wakati 
kila klabu ilipata sh. 7,242,252.45. 
Wamiliki
 wa uwanja walipata sh. 3,682,501.25, gharama za mchezo sh. 
2,209,500.75, Bodi ya Ligi sh. 2,209,500.75, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira
 wa Miguu (FDF) sh. 1,104,750.37, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar 
es Salaam (DRFA) sh. 859,250.29.




 
 
 
 
 
 
 


0 maoni:
Post a Comment